HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 May 2013

ZINEDINE ZIDANE NI MSHIRIKA WA KWELI :FROLENTINO PEREZ


 

Zidane anaoneka kumvutia sana Rais wa klabu ya Real Madrid ya Uispania na wanatarajia kufungua mradi wa soka hivi  karibuni. 

Mfaransa hyuo ambaye anamalizia masomo yake wiki ijayo baada ya miaka miwili ya masomo katika jiji la  Limoges na Paris  .Anafanya Vizuri kwa sasa kwani atakuwa amejianda vya kutosha kuhakikisha kuwa anapata ujuzi zaidi katika kuongoza taasisi za kisoka kwani amejifunza pia mambo uchumi na masoko bila kusahau mawasiliano kwa maana ya Mahusiano
.
Ukiachana na uzoefu wake kiwanjani ,Mchezaji huyu wa zamani wa Real Madrid anataka pia kuelewa jinsi ya kufanya biashara ya namna gani awe na uwezo wa kuzungumza na Mawakala na kufanya Majadiliano ya Kibiashara na Mikataba ya Wachezaji.
Msimu wa ligi utakapo kwisha  Zidane anajua cha kufanya  Nia yake hasa ni kuwa Mkufunzi lakini hilo linawezekana pale ambapo uchaguzi utafanyika kwani Rais wa sasa Florentino Pérez anataraji kugombea tena uenyekiti wa klabu hiyo .
Zidane ni moja kati watu wanaoaminiwa zaidi na Rais huyo wa  Real Madrid , Na pindi uchaguzi utakapo kwisha na kupata matokeo yake ndipo mustakbari wa Zidane utakapojulikana  ,Lazima watu wakumbuke kuwa Perez hajaacha kuwasiliana na Zidane ambaye alimsainisha mwenyewe mwaka   2001 wakati wa kiangazi.
Tangu wakati huo maswahiba hao wawili wamekuwa wakafanya kazi  pamoja na kutaka kuifanya Real Madrid kuwa timu bora zaidi Duniani  .
 Florentino  amekuwa akifuata ushauri wa zidane na wamekuwa wakishauriana , na sasa tunatarajia kumuona  Zidane katika mtazamo mpya . na tunaamini kuwa atafanikiwa kuleta juu yale ambayo anafikili yatakuwa safi katika soka hasa katika uchumi na Masoko kwenye soka

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers