HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 May 2013

Friends Rangers,Mpwapwa Stars YAFUZU HATUA INAYOFUATA BILA JASHO


 
Wakati Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaanza kutimua vumbi keshokutwa (Mei 12 mwaka huu), timu mbili zinakwenda moja kwa moja raundi inayofuata baada ya mabingwa wa Pwani, Kiluvya United kuondolewa na mkoa wa Manyara kutowasilisha bingwa wake.


Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 10 mwaka huu) imeiondoa Kiluvya United baada ya kubaini kuwa timu hiyo haikushiriki ligi ya mkoa wala wilaya msimu uliopita, hivyo kutokuwa na sifa ya kucheza Ligi ya Mkoa msimu huu.

Hivyo Friends Rangers ya Dar es Salaam iliyokuwa icheze na Kiluvya United na Mpwapwa Stars ya Dodoma iliyokuwa iwakabili mabingwa wa Manyara zinakwenda moja kwa moja raundi ya pili.

Timu nyingine iliyokwenda moja kwa moja raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 25 na 25 mwaka huu na mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu baada ya kupita kwenye upangaji ratiba ni mabingwa wa Shinyanga, Stand United FC.

Kamati hiyo iliyokutana chini ya uenyekiti wa Blassy Kiondo pia imeagiza viongozi wa mikoa ya Manyara na Pwani waandikiwe barua za onyo kwa kushindwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao.

Vilevile imesisitiza viwanja vitakavyotumika kwa mechi za RCL ni vya makao makuu ya mikoa tu, isipokuwa kwa Uwanja wa CCM Mkamba ulioko Ifakara, Morogoro ambao ulishakaguliwa na TFF, hivyo kutumika kwa michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu. Pia usajili unaotumika katika RCL ni ule ule wa ligi ya mkoa.

Mechi za Mei 12 mwaka huu zitakuwa kati ya Kariakoo ya Lindi dhidi ya Coast United ya Mtwara (Uwanja wa Ilulu), Techfort ya Morogoro vs African Sports ya Tanga (Uwanja wa CCM Mkamba), Machava FC ya Moshi vs Flamingo SC ya Arusha (Uwanja wa Ushirika), Simiyu United ya Simiyu vs Magic Pressure ya Singida (Uwanja wa Simiyu) na Polisi Jamii Bunda ya Mara vs UDC ya Mwanza (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume).

Polisi SC ya Geita vs Biharamulo FC ya Kagera (Uwanja wa Geita), Saigon FC ya Kigoma vs Milambo FC ya Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika), Katavi Warriors ya Katavi vs Rukwa United ya Rukwa (Uwanja wa Katavi), Njombe Mji ya Njombe vs Mbinga United ya Ruvuma (Uwanja wa Sabasaba) na Kimondo SC ya Mbeya dhidi ya 841 KJ FC ya Iringa (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).

Mechi kati ya Red Coast na Abajalo itachezwa Mei 13 mwaka huu Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Mei 12 mwaka huu uwanja huo utatumika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Mgambo Shooting.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers