HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 May 2013

CHANETA YAMKANA RASMI MMALAWI Marry WayaKocha wa timu ya taifa ya mchezo wa pete Marry Waya   amerpotiwa kuwa hana kandarasi yoyote na timu hiyo na inasememkana ulikwisha malizika tangu mwaka jana ,
kwa mujibu wa mwenyekiti mpya wa CHANETA  aliyechaguliwa hivi karibuni  , Anna Kibira amethibitisha swala hilo hapo jana .
Akiongea kwa simu katika mahojiano jana , Kibira amesema kuwa hakuna takwimu yoyote inayoonyesha kama kocha huyo alikuwa na kandarasi au data zozote zinazoonyesha kulikuwa na kazi zozote inazobidi zifanyike na kocha huyo mpaka sasa au hapo badae  .

amesema litakuwa jukumu la kamati yake kuchagua kocha mpya au kuifundisha timu hiyo na ambaye atakuwa kocha wa kimataifa au kutoka nyumbani
.katika majarada tuliyopewa na uongozi uliopita hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa
“ Marry Waya ni kocha wa timu ya taifa ya mpira wa pete na hakukuwa na kunaonyesha kama kuna jukumu lolote la kimataifa litafanyika,” .

Je kuna uwezekano mkahitaji Huduma zake ?Kibira ", tutalizungumzia hilo pale kamati yetu ikapokaa mwishoni mwa mwezi huu jijini  Dar es Salaam kabla hatujakwenda kuzungumza na wenzetu wa  Zanzibar ambapo ndipo yalipo makao makuu ya CHANEZA , Ndipo tutakapozungumzia kama kuna uwezekano wa kutafuta kocha mwingine au kundelea na   Waya.

aidha mambo mengine yatakayo zungumziwa ni kuhusu kuajiriwa kwa katibu mkuu wa chama hicho .

Kibira amesema kuwa baada ya kukubaliana na kocha watawasilisha kwa balaza la michezo la Tanzania kwa mtu ambaye atakuwa anafanya kazi kwa muda wake wote kwa ajiri ya chama hicho .

aidha watazungumzia kuhusu uwakilishi wa tanzania katika mashindano ya afrika mashariki na kati yatakayo fanyika mwezi june nchini Kenya.

  Aidha John Chalukulu, ambaye ni moja kati ya watu wanaoshughurikia kazi mbalimbali za balaza la michezo Tanzania amesema kocha huyo alikuwa akilipwa na uongozi uliopita   CHANETA na sio serikali kama inavyofikiliwa .

lakini kwa upande inaonekana kuwa kocha huyo aliazimwa kutoka kwa timu ya Anna Bayi ambaye alikuwa akifundisha timu yake Bayi amesema kuwa endapo serikali itamwajiri kocha basi itabidi ajiuzulu kuifundisha timu na kama haitamwajiri basi ataendelea kuifundisha timu yao
kocha huyo ambaye aliazimwa na chaneta aliisaidia timu mashindano ya mataifa sita yaliyofanyika nchini singapore ambapo ushindi huo uliiisaidia Tanzania kupanda katika viwango vya (INF).

Waya Alikuwa akiziba  nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Marry Protas, mmalawi huyo aliisaidia timu ya Filbert Bayi kushinda mashindano ya ubingwa wa tanzania yaliyofanyika  Mbeya mwaka jana . 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers