HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 May 2013

TANZANIA YAANZA KUJIKAKAMUA NA OLIMPICK YA BRAZIL


 

Tanzania imeanza maandalizi ya kuwania kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil kwa kuanza kuwapa mafunzo ya kimataifa walimu wa mchezo wa mpira wa wavu ili wasaidie kuinua kiwango cha mchezo huo .
Mafunzo hayo pia yanatolewa kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 na kuendelea kwa lengo la kuepuka kuitwa wasindikizaji katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika mwaka 2016.

Lina Kessy, mratibu wa mafunzo ya walimu wa mpira wa wavu yanayoendelea mkoani  Tanga, amesema  mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu wa shirikisho la kimataifa la mpira wa wavu kutoka nchini Uingereza na kusimamiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

Kessy alisema lengo kuu ni kuimarisha viwango vya mchezo wa mpira wa wavu nchini na kuwaandaa wachezaji hao ambao bado wana nguvu kulingana na umri walionao.

“Tumeanza maandalizi sasa ili kuwajengea uwezo vijana hawa wajiamini lakini pia watambue nafasi yao iko wapi katika mchezo huu hivyo wapo wataalamu kutoka nje ya nchi ambao wanawapa uzoefu,” Kessy.

Naye rais wa chama cha mpira wa wavu nchini (TAVA), Augustino Paul 'Agapa', amesema mara baada ya mafunzo hayo walimu watapewa vyeti maalum vinavyotambulika na shirikisho la mpira wa wavu duniani pamoja na kupata fursa ya kufundisha mchezo huo katika nchi mbali mbali kwa kutumia vyeti hivyo.

Awali akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Chiku Gallawa, alivitaka vyama vya michezo nchini kutumia vizuri fursa za Rais Jakaya Kikwete za kuwaletea walimu wa michezo katika kuimarisha viwango vya michezo nchini hasa kwa kutambua kuwa Rais alitoa ofa kwao ambayo hadi sasa hawajaifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers