HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 May 2013

JE NINI MAISHA YA BAADAE YA MRISHO NGASA WA SIMBA ?

Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao.
 Kwa hari isiyokuwa ya kutegemewa kabisa katika uwanja wa taifa hapo jana mchezaji wa zamani wa klabu ya yanga ambaye kwa sasa anachezea klabu ya simba Mrisho Ngsa alionekana kubebwa na Mashabiki waliovalia jezi ya klabu ya yanga yenye maskani yake Jangwani.
 Mrisho ngasa aliwahi kuchezea klabu hiyo na baadae kuhamia Azam fc ambapo alikaa katika klabu hiyo zaidi ya miaka mitatu lakini alionekana kubusu jezi ya Yanga wakati akichezea klabu hiyo ya azam fc katika michuano ya kombe la kagame lakini kabla ya mechi ya jana kulikuwa na tetesi nyingi zikimuhusisha mchezaji huyo kurejea katika klabu yake ya zamani yanga .

Habari ambazo zilizua minong'ono kadhaa katika vyombo vya habari na majibizano ya baadhi ya viongozi wa timu zote mbili .kama ilivyokuwa siku ya kubusu jezi ya yanga ilionekana ni mwiba mchungu kwa Azam ambao hawakufurahi kabisa kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi hiyo ilighari akiwa amevalia jezi Azam fc.

Lakini jana mara baada ya mpira kumalizika mchezaji huyo alionekana kubebwa na Mashabiki waliovalia jezi ya mabingwa wa ligi ya soka ya kandanda Tanzania bara Dar es salaam young afrika 


Mashabiki wa Yanga wakiwa wamembeba mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa mara baada ya mpira kumalizika, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika klabu yao.

Hili sio jambo Rahisi katika klabu za  mpira wa tanzania hasa kwa timu ambazo zinazidi kushika umaarufu katika soka ya afrika Mrisho Ngasa anaweza au mashabiki hawa waliombeba wanaweza kuona wamefanya jambo dogo  au wanajua kabisa Tukio wanalolifanya sasa' linaweza kuzua mijadara mbalimbali katika vyombo vya habari hasa ukizingatia ni timu mbili pinzani 
kwa upande mwingine ni tofauti sana na nchi zilizo endelea kuona tukio kama hili wapo wachezaji duniani ambao wanaweza kuhamia timu pinzani lakini wakaweka heshima na kutokuonyesha dalili za aina yoyote kama kuna mahusiano ya wao kuhamia timu pinzani.

kwa umma wa watanzania na mashabiki wengi wanajua fika kuwa Ngasa bado yupo simba bila kuona nyaraka za utiaji saini kwani isingekuwa hivyo tff isingemrughusu kuchezea simba lakini tutazame kwa sasa picha hii inayoonekana sasa ina maana gani kwa ngasa mwenyewe ,mashabiki wa timu zote mbili pamoja na viongozi wa timu zote ,Ngasa anaoneakana Mwingi wa tabasamu sana usoni lakini ataaendelea kutasabasamu mpaka mwisho Mrisho ngasa aliondoka yanga baada ya kuoneakana kwenda rwanda kujaribu kuchezea APR kocha mkuu wa yanga wakati huo  alikuwa Dusan Kondic ambaye kwa mujibu wa mwenyekiti wa yanga wakati huo imani madega alisema kocha ameona ni kheri wamuuze huyu alikuwa ni mkufunzi wa kigeni 
na wakati alipokuwa Azam fc alikuwa chini ya Sterwart Jonh hall ambaye hakulalamika sana kwa mchezaji huyo kuperekwa simba japokuwa ilisemekana kuwa alikwenda kwa mkopo huku baadaae ikidaiwa mchezaji huyo ameingia kandarasi ya muda mrefu hapa nikutaka kukuonyesha farsafa za makocha wa kigeni zilivyo jambo rahisi zaidi ni kwamba hatutashangaa sana kuona Mfaransa huyo wa simba Patrick Liewing akiridhia Ngasa kuondoka .
  kama atafanikiwa kurejea Yanga je ni upi utakuwa mustakbali wa maisha ya kisoka ya mchezji huyu wa simba kwa sasa pengine hata kama ana mapenzi na Yanga kulikuwa na haja gani ya kuonyesha dhahiri kiasi kile  hasa katika mechi ambayo unacheza timu pinzania na unayopipenda au ndio kujiwekea maandalizi ya kuondoka au kutaka ufukuzwe urejee timu yako ya zamani .

kwa hakika wapo wachezaji wengi wenye mapenzi na timu zao binafsi kiasi kwamba hata kama akicheza nayo huendelea kuifunga kama kawaida lakini je ni kweli kuwa  ngasa hakuataka kuifunga yaga jana tena kwa penati ambayo alifanyiwa faulo yeye mwenyewe kwa sasa Tanzania inatakiwa kutizama mafuzno ya  kweli ya mpira wa kulipwa kwani kimaitafa wanaposema mpira wa kulipwa hawazungumzii fedha." hata tabia kiwanjani na jinsi unavyoewa kuishi na wachezaji wengine na mashabiki wa timu tofauti na wewe  ,
JE NINI MAISHA YA BAADAE YA MRISHO NGASA WA SIMBA  


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers