HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

31 May 2013

MANGWEHA KUAGWA VIWANJA VYA LEADERS

HUKU wakikanusha ripoti  za awali zinazoendelea kusambaa juu ripoti ya kifo cha msanii Albert Mangwea, Kamati ya Mazishi ya msaniii huyo, imesema kuwa inatarajia kuuleta mwili wa marehemu huyo kesho kama ilivyopangwa na kuuaga Jumapili katika Viwanja vya Leaders Club, baada ya kulala katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa siku moja.
                                 Marehemu Mangwea
Mangwea moja ya wasanii nyota hapa nchini alifariki nchini Afrika Kusini na kuzua huzuni kubwa kwa wadau wa muziki na Watanzania kwa ujumla, hasa kutokana na umahiri wake kwenye kazi hiyo, huku kifo chake kikipokelewa kwa masikitiko makubwa mno na redio zote kusikika mara kwa mara nyimbo zake zikipigwa kama sehemu ya kuomboleza msiba wa msanii huyo nyota.
Mara baada ya kuwasili kesho, mwili wa marehemu utafikia kwanza katika Hospitali ya Muhimbili huku siku inayofuata ratiba zilizopangwa kuendelea kwa ajili ya kuustili mwili wake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Kamati iliyoundwa ya kuratibu shughuli zote za msiba huo, Adam Juma, alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya kuleta kwa mwili huo na utaratibu mzima wa maziko yake yanaendelea.
Alisema ili waweze kufanikisha suala hilo, wanaomba msaada wa Watanzania bila kubaguana kwa namna yoyote, maana Ngwea alikuwa mtu wa watu, hivyo hakuna haja ya kuleta propaganda katika suala hilo.
“Tunakabiliwa na changamoto nyingi katika msiba huu, hivyo tunawaomba Watanzania wenzetu waweze kuchangia kwa namba ya Vodacom, 0754 074323 au Tigo 0658 074324 ambazo fedha zote zitaingia kwenye simu za kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea, ambaye ni kama mwenyekiti katika Kamati hii ya kuratibu mazishi ya msanii huyu.
“Kuna vitu vingi vya kufanya na vyote vinahitaji gharama, kama vile kuleta mwili wake, kuuaga sambamba na usafiri wa ndani, bila kusahau safari ya kuelekea Morogoro kwa ajili ya maziko yake,” alisema.
Aidha, Kamati hiyo inayoongozwa na Shirikisho la Muziki Tanzania, chini ya Rais wake, Addo Novemba, ilisema kuwa ripoti iliyoanza kutolewa jana kwenye mitandao ya kijamii si ya kweli.
“Tunaomba Watanzania tuendelee kuwa na subira katika suala hili, maana ripoti iliyosambazwa kwenye mitandao si ya kweli na imeletwa kwa ajili ya kumdhalilisha marehemu Ngwea,” alisema Novemba.
Msiba wa Ngwea umepokelewa kwa masikitiko makubwa na Watanzania, hasa kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, akitamba na nyimbo nyingi, kama vile Gheto Langu, Mikasi, Speed 120 na nyinginezo lukuki.
Aidha, mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva nchini, P-Funk, amefunga mdomo kuelezea kwanini aliamua kuwapiga marufuku redio ya Clouds FM kucheza nyimbo alizorekodi yeye na kuimbwa na marehemu Ngwea enzi za uhai wake.
"Kwa sasa sitaki kusema lolote juu ya nyimbo hizo za Ngwea kuchezwa au kutochezwa Clouds FM," alijibu kwa kifupi akiwa na maana ya kuelekeza akili yake kwenye msiba wa msanii Ngwea.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers