HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 May 2013

MKASA WA Judith Wambura ( Lady JayDee) WAFIKA PABAYA SASA !!!

 Na Andrew Chale 0719 07 63 76
MWANAMUZIKI nguli wa bongo na kiongozi wa yenye mvuto nchini bendi ya ‘Machozi’,  Judith Wambura ( Lady JayDee) au  Jide ama #Teamaanaconda#,  anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni siku ya Jumatatu Mei 13, kufuatia kufikishiwa kwa taarifa hizo Gadna G Habash ‘Captain’ ambaye ni Meneja na mumwe wa Lady Jay Dee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mchana wa leo, Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa kwa Lady Jay Dee kufika Mahakama ya Kinondoni, siku ya Jumatatu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni,  Hii ni kufuatia kwa jana  kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo na walikuja na barua ya kumkabidhi Lady Jay Dee mwenyewe hata hivyo hawakumkuta” alisema Gadna.
Aliendelea kueleza kuwa, hata alipowaeleza watu hao wamkabidhi yeye hiyo barua watu hao walisema ilikuwa si lahisi zaidi alitakiwa akabidhiwe mlengwa, hivyo kumueleza kuwa wito wa kufika mahakamani siku ya Jumatatu, na  aliwakubalia kwa hilo.
Hata hivyo, Gadna alisema hajajua Lady Jay Dee anaitiwa nini na kwa sababu ya nani zaidi amemwelezea na amesema watatekeleza wito huo wa kufuka Jumatatu Mahakamani hapo.
Aidha, kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa facebook,  Lady Jay Dee aliandika: “Ratiba ya Usiku wa leo,  ni Machozi Band, kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea...” aliandika Jide  kwenye ukurasa huo ambao mpaka hatua ya mwindishi anatembelea ‘post’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ambayo watu mbalimbali walipata kuchangia.
Maoni hayo yanayokaribia zaidi ya 558 na, ‘Like’ zaidi ya 756 na ‘Share’ zaidi ya 20,  ambapo wengi wao wameweza kumuhusisha moja kwa moja na Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba kuwa ndie aliyefanya hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na moja ya gazeti hivi karibuni ilimnukuu Ruge kuwa amejiandaa kuchukua hatua  ikiwemo ya kisheria dhidi ya Lady Jay Dee baada ya kumsema kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
**
Aidha, katika kuelekea shoo yake ya Miaka 13 ya Lady JayDee, amemtangaza rasmi msanii machachali wa bongofleva, Juma Nature.
Jide alisema Nature ameongezeka katika list ya wasanii watakaokuwepo kushiriki miaka 13  ambapo ataungana na wasanii wengine wengi siku hiyo  ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa. “Naomba mujitokeze kwa wingi na tiketi zinapatikana karibu sehemu zote ikiwemo Shear Illusions Mlimani City, City Sports Lounge Mjini Posta, BM Salon Kinondoni, American Nails n Hair Salon,  bila kusahau Nyumbani Lounge mahala patakapofanyika shoo hiyo

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers