HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 May 2013

RAIS KIKWETE" MKISHINDA TUTAFURAHI SANA NA MKISHINDWA TUNANYONGEA SANA "


Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo  mingine  ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya  kushiriki  mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014. Picha na 2 
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo  mingine  ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya  kushiriki  mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014. Picha na 4 
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia. Picha na 5 
Meneja wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete. Picha no 3 
Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars wakipata chakula walichoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo alipokutana nao kuwatakia ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco. Picha na 6 
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Picha na 7 
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO na Freddy Maro Ikulu.

Na Veronica Kazimoto –MAELEZO
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo dhidi ya timu ya taifa ya Moroco mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia  2014 nchini Brazil .
Rais Kikwete amewaambia wachezaji wa timu  hiyo kuwa ina uwezo mkubwa  wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao  dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata  ushindi wa bao 2-0.
 “Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tutafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,”  Kikwete.
 Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen  pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia  na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.
 Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.
 Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake nahoidha wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi  kwenye mechi zijazo.
 Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers