HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

31 May 2013

SIMBA YANASA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SAIGON XUAN THANH YA VIETNAM

 Mchezaji wa kimataifa wa uganda Uganda Cranes  Moses Oloya huenda akatua nchini muda wowote kutoka sasa akiwa mbioni kujiunga na simba.
Simba ambao msimu huu wameshindwa kutetea  ubingwa , wanajiandaa na michuano ya  Cecafa Kagame Cup, iliyopangwa kuafanyika Sudan Mwezi ujao .
Timu hiyo  bado inajiandaa kwa msimu ujao na bado inatafuta wachezaji wengine baada ya winga wao machachari Mrisho Ngassa ambaye amejiunga na  mabingwa wapya wa ligi ya  Tanzania Yanga.
 kamati ya simba ya usajiri inayoongozwa na  Zacharia Hanspoppe amethitisha kuwa majadiriano yanaendelea mchezaji huyo pia yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya cranes 

Oloya, -ambaye ni mchezaji wa  Saigon Xuan Thanh kutoka  Vietnam,Mchezaji huyo  atajiunga na simba baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Libya na ile ya kuwania kufuzu kombe la dunia mwezi ujao  .
sasa ataungana na mchezaji mwenzake  Samuel Ssekoom mchezaji wa zamani wa (URA) ambaye naye amesaini kuchezea klabu hiyo .
Simba sasa inawachezaji watano wa kigeni na hii ina maana kuwa watatakiwa kupunguza baadhi ya wachezaji ili kutimiza sheria ya wachezaji wa tano wa kimataifa wachezaji hao  ni pamoja na Mlinda mlango  Abel Dhaira (Uganda), Felix Sunzu (Zambia) na  Mude Mussa kutoka Uganda.
Timu hii tayari imeshamaliza kazi ya kusajiri beki  Issa Rashid, Mlinda mlango  Andrew Ntalla, Mshambuliaji  Zahor Pazi na kiuongo  Twaha Shekuwe.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers