HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 May 2013

Sir Alex Ferguson ASHUSHA MAPATO MANCHESTER UNITED


Huku maelfu wa mashabiki wakionekana kushtushwa na habari za kustaafu kwa Fergie maarufu kama babu, lakini pia upande wa masoko kwa klabu ya Manchester United kumekuwa na pigo pia.
Hii ni baada ya kushuka kwa ununuzi wa hisa za klabu hiyo kwa zaidi ya asilimia tano kwenye soko la hisa la New York.
Wachambuzi wa masuala ya biashara wameeleza hofu yao juu ya kushuka kwa biashara za United kufuatia kuondoka kwa Ferguson kwa kusema itakuwa kazi kubwa kumpata mrithi wake ambaye ataweza kuchagiza mafanikio ya klabu hiyo yatakayovutia wadhamini mbalimbali kama alivyofanya kwa miaka 27 aliyokaa na United.
Familia ya Malcom Glazer yenye makao yake Miami nchini Marekani ambayo ndio inayomiliki klabu ya Manchester United bado haijatangaza mrithi wa Ferguson japo wadadisi na vyanzo vya karibu vya United vinasema huenda kocha wa Everton, David Moyes atakabidhiwa jukumu la kuifundisha United,taarifa ambazo hazijathibitishwa wala kukanushwa na uongozi wa Old Trafford.
Kushuka huko kwa hisa za United kumeifanya klabu hiyo kupoteza mapato yake kwa karibu asilimia 1.3 kwa hisa moja ambayo hununuliwa kwa dola za kimarekani 18.52 kwa hisa.
Licha ya kushuka kwa hisa hizo kufuatia taarifa za kustaafu kwa Ferguson lakini zaidi ya asilimia 30 ya hisa za United ziliuzwa kwenye soko la hisa hii leo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers