HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 May 2013

TENNIS PARALYMPICS KUELEKEA ANTALYA JUMAPILI IJAYO


 
Timu ya taifa ya walemavu ya mchezo wa mpira Tennis wanaotumia viti vya matairi inaondoka jumapili ijayo kwenda nchini uturuki kushiriki michuao ya  BNP Paribas ambayo ni michuano ya dunia itakayo fanyika katika jiji la Antalya michuano hiyo itafanyika kuanzia  May 20-26.

Kamati ya mchezo ya walemavu ya Tanzania Paralympics  (TPC) inayoongozwa na Mwenyekiti , Johnsen Jansen, Amesema kuwa wachezaji wawili wataiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo.
wachezaji hao wataambatana na maafisa wawili .

wachezaji ni pamoja  Novatus Emmanuel anayetoka shule ya  Pugu Secondary na  Juma Hamis wakati watakaongozana nao ni pamoja na  Mathew Selevani na Mkufunzi wa Timu  hiyo Riziki Salum.

Michuano ya BNP Paribas kwa walemavu inaenda sawa kwa viwango na Davis Cup na  Fed Cup katika hatua za kimataifa .

“Hii ni mara ya kwanza tutakuwa na timu katika mashindano ya timu za kimataifa .Wachezaji hawa walipata vigezo vya kushiriki michuano hii baada ya kufuzu katika mashindano yaliyofanyika nchini kenya nchini mwaka jana  .
“.Tuna amini kuwa tutarudi na Nishani,” .Mashindano ya  BNP Paribas ni mashindano ambayo hufanyika kila mwaka katika nchin tofauti na hujumuisha nchi mbalimbali na hujumusiha wanawake na wanaume katika viwango na miaka tofauti  mbali.

“Aidha alimshukuru ,  Inga Njau kwa kuwaunganisha na shirikisho la mchezo wa Tennis .Bila yeye tusingekuwa hapa,
 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers