HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 May 2013

TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA MAGONGO KUSHIRIKI MICHUANO YA MATAIFA YA AFRIKA KENYA MWEZI SEPT


 

Timu ya mchezo wa mpira wa magongo inatarajia kushiriki michuano ya mataifa ya afrika ndani ya mwezi Tisa  mwaka huu , Katibu mkuu wa wa chama cha mpira wa Magongo , Kaushik Doshi, amesema .

Doshi ameongeza kuwa mashindano ilibidi ya fanyike nchini Misri lakini sasa yatafanyika nchini kenya kuanzia September 26 up to October 5.

Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa golf nchini kenya amesema kuwa mashindano hayo yatatoa washiriki watoakwenda kushiriki michuano ya kimataifa ya dunia ya mchezo huo mwaka 2014 .
ambapo mashindano yaliyopita yalifanyika nchini   Zimbabwe  2011 aidha afrika kusini ilifuzu kucheza mashindano ya kimataifa sanjari a Misri
“Tutashiriki michuano ya mataifa ya afrika,ambayo Kenya inashikirikiana na shirikisho la mpira wa Magongo la afrika vile vile na shirikisho la kimataifa la mpira wa magongo,” .

Ameongeza kuwa watapereka jumla ya wachezaji kumi nane ambao watashiriki katika makundi mawili ya wanawake na wanaume.

  Ameyaomba makampuni, Taasisi mbalimbali na watu binafsi kukisaidia chama hicho hata vifaa ili iweze kushiriki na kujiandaa michezo hiyo .

“Chama chetu akina fedha za kuandaa timu na kuipereka timu kenya ni gharama kidogo kwa ajiri ya mashindano hayo. Tungependa kuwaomba wale wote ambao watakuwa wamehamasika kwa upande mmoja au mwingine pamoja na washika Dau tuna wakaribisha katika kuichangia timu yetu .Mchango wao utasaidia kuinua mchezo wa magongo nchini  ,”Kaushik Doshi .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers