HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

14 May 2013

ZAMALEK NA AL AHLY KUNDI MOJA KWA MARA YA PILI KLABU BINGWA AFRIKA



 
Kwa mara ya pili na kwa mwaka wa pili tena mahasimu wa soka la Misri  Zamalek na Mabingwa watetezi  Al Ahly wamewekwa tena katika kundi moja katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani afrika maarufu kama Orange CAF Champions League katika ratiba iliyopangwa leo katika makao makuu ya CAF huko Cairo. Mafahari hao wawili wa misri wapo kundi A na watakutana  katika mechi ya ufunguzi wa makundi hayo ambayo ndiyo itakayo kuwa mechi ya kwanza Tarehe 19-21st Mwezi July huku  Zamalek wakiwa wenyeji wa mchezo huo . na mabingwa wa mwaka 1995 Orlando Pirates wataialika  AC Leopards ya jamhuri ya kidemoklasia ya watu wa  Congo katika mchezo wa kundi A .
 
 
Kocha msaidizi wa  Zamalek, Ossama Nabuih amesema kuwa  sio jambo la kushangaza kuwa kundi moja na mahasimu wao wakubwa  Al Ahly kwa mara ya pili . “ tuliitarajia ratiba hii . hakuna kusema kuwa kundi hili ni rahisi au ngumu . Kwa hatua hii kila kundi ni gumu tuna kwenda kucheza kwa kujiamni na tutafuzu katika kundi hili ” . kundi letu ni gumu kuliko jingine  . Tutakutana na timu ngumu kutoka katika mataifa tofauti .anamaliza  Nabuih          
 
 
Group A
Al Ahly  (Egypt)
AC Leopards (Congo)
Orlando Pirates (South Africa)
Zamalek (Egypt)
 
 
Group B
Esperance (Tunisia)
Coton Sport (Cameroon)
Recreativo de Libolo (Angola)
Sewe Sport (Ivory Coast)

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers