HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

1 June 2013

BERNAD MEMBE AISHANGAA CECAFA KUPELEKA KAGAME DARFUL


 

Waziri wa mambo ya nje Bernad Camilius Membe amelishngaa baraza la vyama vya soka afrika mashariki na kati CECAFA linaoongozwa na rais aliyemaliza muda wake tff Leordgar chila Tenga kwa kupeleka mashindano ya cecafa Sudan kusini hasa katika jimbo la Darful kuwa ni kitendo cha kushangaza sana membe alikuwa akijibu swali lililoulizwa na moja ya mbunge katika majadiliano ya wizara mambo ya  nje.

Membe anasema kuwa anshangaa sana tena ikiwezekana atapiga marufuku timu za simba na yanga kwenda kushiriki mashindano huku akisisitza kuwa Darful hakuna hotel  viongozi na baadhi ya mabalozi ambao wanakwenda huko hupokewa kwenye mabasi ambayo hayapitishi risasi ili kuwaweka katika hari ya usalama .

Membe anaongeza kwa kusema atakwenda kuzungmuza na mamlaka husika kuzungumza nao ni kwanini wamepeleka mashindano huko sehemu ambayo ni hatari kwani kufanya hivyo ni fedheha kwa taifa kupeleka wachezaji sehemu amabayo hakuna usalama kwa sasa .

Timu za simba na yanga zitaiwakilsiha tanzania bara  katika mashindano hayo yatakayoa aanza hivi karibuni  zikiiwakilisha tanzania na kama serikali itazuia basi huenda hata zanzibar inaweza isipeleke timu kutoakan hari ya kiusalama  

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers