HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 June 2013

MALAWI 2-2KENYA ,NIGERIA IKISHINDA USIKU HUU DHIDI YA NAMIBIA ITAFUZU HATUA YA MTOANO

Late own goal sees Malawi heldTimu ya taifa ya soka za Taifa za  Malawi na Kenya zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2 mjini Blantyre katika  mechi ya kufuzu kombe la dunia.
Malawi walikuwa wanaongoza mabao  mawili kwa moja lakini katika dakika ya mwisho Chimango Kayira alijifunga na kupunguza  uwezekano wa Malawi kusonga hatua inayofuata.

The Flames ndio waliowakwanza kupata  bao katika  dakika ya 46, bao lililofungwa na Robion Ngalande, lakini dakika sita baadaye Mohamed Jamal akaisawazishia Harambee Stars.
Katika dakika ya 81, Robert Ng'ambi alifunga bao la pili la Malawi, kabla ya Kayira kujifunga na mechi kumalizikia mabao mawili kwa mawili.
Matokeo hayo yana maana kwamba mabingwa wa Afrika Nigeria ndio watakaofuzu hatua inayofuata kutoka kundi la F, ikiwa wataishinda Namibia mjini Windhoek, mechi inayochezwa baadaye usiku huu.
Hdi kufika kuna bakia mwaka mmoja  , kabla ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kuanza nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers