HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 July 2013

KLABU NNE ZAPIGWA MARUFUKU NIGERIAMuke Umeh, mwenyekiti wa kamati andalizi ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria NFF

Vilabu vinne ambavyo vilihusika na njama ya kupanga matokeo ya mechi vimepigwa marufuku nchini Nigeria.
Katika mechi moja klabu moja iliilaza nyingine magoli 79-0 na magoli 67-0 katika mechi ya pili.
Jumla ya magoli 146 zilifungwa katika mechi hizo mbili, idadi ambayo inaingia katika vutabu vya kumbukumbu kama mechi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya magoli duniani.
Klabu ya Plateau United Feeders iliilaza timu ya Akurba ili hali timu ya Polisi ya Machine FC kwa upande wake ikailaza Bubayaro magoli 67-0.
Mwenyekiti wa kamati andalizi ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Muke Umeh amesema ufisadi na ulaghahi wa kiwango hicho hakiwezi kukubalika katika soka ya sasa.
Umeh ametangaza kuwa baada ya mkutano wa kamati hiyo, ilibainika wazi kuwa vilabu hivyo vina kesi ya kujibu na hivyo vyote vinne vimepigwa marafuku ya kushiriki katika mecho yoyote, hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mchezo unaopendwa na wengi

Mechi ya soka katika mtaa mmoja nchini Nigeria
Kabla ya mechi hiyo vilabu vya Plateau United Feeders na Police Machine vilikuwa na alama sawa na vilikuwa vikipania kupandishwa daraja hadi ligi daraja ya pili.
Feeders ilipata magoli 72, katika kipindi cha pili ili hali Machine nao wameripotiwa kufunga magoli 61 katika kipindi cha mechi yao.
Kufuatia matokeo hayo Plateau ilimaliza ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na idadi kubwa ya magoli ikifuatwa na timu hiyo ya polisi.
''Tutachunguza sakata hii na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika'' Alisema Ummeh.
Mkurugenzi wa michezo na mashindano wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Dkt. Mohamed Sanusi, amekariri tangazo lililotolewa na mwenyekiti wa kamati andalizi kuwa waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NFF, vilabu vilivyohusika, wachezaji,, maafisa wa kiufundi wa timu na wasimamizi wa mechi hiyo watakaopatikana kuhusika kwa njia moja au nyingine, katika kashfa hiyo ambayo imetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya soka nchini Nigeria watachukulia hatua kali za kisheria.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers