HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 August 2013

Extra Bongo kutambulisha wapya Mamaz & Papaz Kigamboni

 
 
 Na Mwandishi Wetu :WAKALI wa muziki wa dansi nchini Extra Bongo 'Next Level Wazee wa Kizigo' keshokutwa Alhamisi wanatarajiwa kuwatambulisha wanenguaji wake wapya wawili iliyowatwaa kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) katika onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa Mamaz & Papaz Kigamboni jijini Dar es Salaam. 
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, msemaji wa bendi hiyo, Juma Kasesa, amesema, kuchukuliwa kwa wanenguaji hao ni sehemu ya mkakati wa Extra Bongo kuzidi kuimarisha safu yake ya unenguaji inayoongozwa na mkongwe Super Nyamwela na Otilia Boniface. Amesema onyesho hilo litakuwa ni maalumu kwa wakazi wa Kigamboni na vitongoji vyake kuona shoo mpya za bendi hiyo zikichagizwa na ujio mpya wanenguaji hao ambao wametokea katika bendi ya Wenge Maison Merre ya Werrason Ngiama Makanda na kwa mwanamuziki Ferre Gorra. 
 
Aliwataja wanenguaji hao kuwa ni Jolie Kindu aka Mrisho Ngassa na Fatuma Grace aka John Bocco ambao mara baada ya onyesho hilo watatambulishwa Ijumaa ndani ya Ukumbi wa Eliada Port View Pugu kwa Mjomba huku Jumamosi zoezi hilo likiendelea ndani ya kiwanja chao cha nyumbani Meeda Club Sinza na kuhitimisha Jumapili kwenye bonanza lao ndani ya jumba la maraha Dar West Park Tabata. 
 
Aliwataka mashabiki na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushuhudia staili na nyimbo mpya za bendi hiyo kama 'Hafidhi' utunzi wa Athanas Muntanabe, 'Mgeni' Khadija Mnoga 'Kimobitel' na 'Wanawake' wa Papii Catalogie.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers