HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 August 2013

KASEJA;NON JE NE PALRE française !!! ANDIKA KINGEREZA

 
Nahodha na Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja ameshindwa kusaini mkataba na timu ya FC Lupopo ya Congo DRC baada ya mkataba kuletwa kwa lugha ya Kifaransa.
Kaseja alikubaliana kila kitu na Lupopo ikiwa pamoja na yale aliyotaka yawekwe kwenye mkataba kabla ya kusaini na kwenda kuitumikia klabu hiyo.
Lupopo wametuma mkataba huo leo lakini imeshindikana kusainiwa kwakuwa upo kwenye lugha ambayo Kaseja ameomba ibadilishwe na kuwekwa kwenye lugha ya Kiingereza ili aone kama alichoomba ndicho kilichoandikwa.

Mkataba huo sasa huenda ukasainiwa kesho kama utakuwa umebadilishwa na Kaseja kuridhika na kile kilichomo ndani ya mkataba.


Kaseja amemaliza mkataba na Simba ambao viongozi wake waliweka wazi kuwa hawataongeza mkataba mwingine na Mlinda mlango huyo aliyedumu zaidi ya miaka 10 kwenye klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers