HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 February 2013

SWANSEA YAFANYA KUFURU WEMBLEY

Swansea's Nathan Dyer (in white) puts his side ahead against Bradford in the Capital One Cup final at Wembley 

Swansea imefanikiwa kutwaa taji lao la kwanza baada ya kuifunga timu kutoka daraja pili ya  Bradford katika fainali ya   Capital One Cup.
  Swans ilikwenda mapumziko ikiwa magoli mawili huku mlinda mlango wa Bradford  Matt Duke kulimwa kadi nyekundu  Nathan Dyer alifunga kwa faulo  kwenye engo ya juu .

League Cup final 
Michu alimiliki mpira kwa miguu yake na baadae  Carl McHugh na  Dyer rifled waliipatia magoli ya kuongoza  Swansea's .

Duke alilimwa kadi nyekundu kwa kumfanyia faulo  Jonathan De Guzman, na alifunga penati hiyo na alifunga tena goli la tano katika dakika za mwisho za mchezo huo na kuipa timu  yake  ushindi timu hiyo inayoshiriki ligi ya uingereza
 
 League Cup final
 

MIWA YA MTIBWA YAMLEWESHA SIMBA



 
 Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa.

Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.

Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezua mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.

Aidha mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku viongozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo. 

Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.

 Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.

 Beki wa Simba Keita, akimdhibiti mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata mabeki wa Simba.
SUFIANI MAFOTO UNDSTAND

SHUGHURI PEVU UINGEREZA CHELSEA CHALI

Yaya Toure celebrates his opening goal

Magoli yaliyofungwa katika kipindi cha pili na  Yaya Toure na  Carlos Tevez yamerejesha ahueni kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya uingereza  Manchester City  baada ya kuikandamiza   Chelsea na kupunguza uwiano wa alama za kuongoza dhidi ya vinara wa ligi ya premier  dhidi  Manchester United kwa alama 12 .
 Frank Lampard alipata nafasi safi ya kufunga goli la mia mbili akiwa na chelsea 200th  lakini penati yake iliokolewa na Joe Hart dakika saba baada ya kipindi cha pili kuanza 

 Yohan Cabaye scores from the spot for Newcastle against Southampton


Newcastle imetoka nyuma mara mbili na kushinda dhidi ya  Southampton.
Morgan Schneiderlin alipiga mpira kwa kuparaza na kuifungia timu yake goli la uongozi  Moussa Sissoko aliisawazishia timu yake kwa kufunga ndani ya kisanduku  .
lakini shuti la mita 25 kutoka  Papiss Cisse  ambaye alifunga bao safi kwa shuti ya aina yake na kuweka mchezo kusomeka moja moja .

Danny Fox's alishika mpira ambao  Yohan Cabaye kwa penati kabla ya  Jos Hooiveld's kujifunga mwenyewe .
mpaka mwisho wa mchezo Newcaslte 4-2soton 

YANGA, AZAM ZALETA MIL 240



Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.

Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers