HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

3 March 2014

MASHABIKI WETU NI WAHUNI AU NI ULIMBUKENI ?

 

 Mpenzi msomaji mwishoni mwa juma hili Mabingwa soka wa Tanzania Dar es salaam young african ilikwaana na Al Ahly katika mechi ya kuwania kwenda mzunguko wa pili wa ligi ya Mabingwa Barani afrika .

sitaki kuzungumzia matokeo ya kiwanja kwani yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa goli moja sifuri lakini cha msingi na kuu kuliko yote hivi ni kweli Tanzania tumefikia sehemu ya kutokea vurugu kiwanjani kiasi hiki?  Hii sio mara ya kwanza kuvunjwa viti kwani sitaki kuihusisha Al AHLY moja kwa moja .

kwani hata ligi za nyumbani yamewahi kutokea haya ,jambo ninalojiuliza hivi kuchukiana kwa simba na Yanga ni kwa kisomi au ni ulimbukeni maana hakuna sababu ya msingi ya kuvunjwa viti mechi hii ilikuwa inahusisha timu moja ya nyumbani na moja  kutoka Misri na kwa hari ya kawaida Al Ahly hutumia jezi nyekundu ambazo kwa Taanzania hutumika na Simba kwa hiyo lazima Al Ahly walipa wafuasi wengi kutoka upande unajulikana kuwa wanakaa mashabiki wa simba na ndiko mashabiki wa ahly walipokuwa wameketi.

Baada ya kukupatia picha hiyo sasa nataka kulitazama tukio hivi hasara hii ya kufanya marekebisho ya kila siku ya kutaka kuhujumu uchumi kila siku itakwisha lini kwani imezoeleka sasa kuwa jambo la kuvunja viti limekuwa  la kawaida, lakini lazima kutazama kwa umakini je simba na yanga tumefikia hapa kwa cha kurushiana viti wenyewe kwa wenyewe ni kweli tumefikia uhuni wa aina hii?  au upeo wetu wa kufikili umefika tamati .

Tanzania hatuna utamaduni wa aina hii sijawahi kuona kiwanjani pengine ingekuwa klabuni ningesema sawa maana kupigana Bakora kwa yanga na simba ni jambo la kwaida lakini sio fujo kiwanjani jambo ambalo limeanza tena kwenye uwanja huu mkubwa wa Taifa ni mambo ambayo tumeyazoea kuyaona katika za america ya kusini Hasa kati ya Riverplate na Boca junior za Argentina lakini sio Tanzania na sitaki kufananisha Argentina na Tanzania katika ulimwengu wa soka ni vitu viwili tofauti.

Tabia hii inayoingia sasa katika soka la tanzania ni mbaya tena hasa katika majukwaa mawili ambayo siku zote yanajulikana yanakaliwa na mashabiki wa timu gani ! ipo siku simba na yanga zitakuja kusabisha matatizo makubwa katika taifa kwani inaonekana dhahiri kunaanza kuingia kwa ushabiki wa kihuni na usio kwenda shule labda kwa wasio fahamau sio viti tu hata vyoo,vioo,na vitu kadhaa vimeshaanza kuharibiwa je ni sahihi kwa sasa kufikia huko ipo sababu ya kulitazama jambo hili kwa upana zaidi .

je tabia hii itakoma lini ?
Ustaarabu huu wa kihuni utakwisha lini ?
kwanini tunakopi mabaya tunaacha mazuri ?
mbona watu weusi waliopo ulaya hawafanyi ushenzi huu ?

Hili ni tatizo la kitabia je Tff na serikali na wanajamii tunalitazamaje?No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers