HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 March 2014

WACHEZAJI WA KITANZANIA KULA KULALA!!



Karibu mpenzi wa kurasa ya yangu kwa heshima na taadhima leo tena nakuelezea kuhusu soka ya Tanzania .
Najua Tanzania ni ambayo mungu kaipenda kiasi kwamba haijawahi kutokea vita ya kutoewana kati ya jamii ya kitanzania tofauti na mataifa mengine ya afrika vita pekee ilipiganwa wakati wa kumtoa Idd Amin rais wa Uganda ambayo Tanzania ilishinda vita hiyo la hasha usininukuu vibaya kuwa nataka tupigane hapana.
Kunatofauti kubwa sana ya wachezaji kutoka afrika magharibi na afrika mashariki  siku zote huwa ninaamini ukiona mchezaji kutoka afrika Magharibi kaja Tanzania kucheza soka huyo sio mchezaji ni skrepa lakini ngoja nije kwenye alama ya msingi.

Wachezaji wetu wa Tanzania wanashindwa kucheza mpira ulaya kwa sababu moja kuu nayo lelemama sio wachezaji wote wa kiafrika ambao wamepita kwenye shule za soka lakini wakafanikiwa kucheza soka, wengi wa wachezaji hawa ni walikubari kulala hata kwenye vituo vya mabasi huko ulaya walikubali hata kufagia barabara za ulaya na wengine kutukanika kufanya hata kazi za kukosha vyombo lakini ukiiosha vyombo afrika utaoneka huna maana chembe.

Wapo wachezaji wa kitanzania ambao wamekwenda ulaya na wameshindwa kusakata kabumbu la ulaya kwa kusingizia ujira mdogo na wengine wakipelekwa hata vikosi vya tatu kufanyiwa marewkebisho lakini wakawaona wazungu wapumbavu sasa kati yao na wazungu nani mpumbavu.
Kikubwa soka ya ulaya bila kujali ligi ni ya nchi gani huwa sio lelemama kabisa kwani mchezaji lazima ukubali kufa  lakini sio kwa wachezaji wa kitanzania ambao wengine wanapata bahati ya kucheza ulaya lakini hawaonyeshi uwezo na matokeo yake huishia kurejea kucheza ligi ya nyumbani ,mchezaji yotote Yule kutoka Tanzania ambaye amekwenda ulaya kucheza akashindwa kucheza huko au kacheza lakini kaamua kurudi nyumbani huyo ameshindwa maisha .

Wapo wachezaji wengi wakitanzania ambao wamecheza nchi za ulaya na America ya kaskazini ambapo ligi zao sio bora kama zile za ulaya lakini wameshindwa kutokana na kushindwa kukomaa na hari ya kimaisha wengi wamekuwa wakitaka mishahara minono tofauti na uwezo wao je unadhani ni rahisi ulaya unalipwa kutoka na kazi unayofanya na ubishi wako kiwanjani.
Wachezaji wanatakiwa kuacha mchezo kiwanjani na sio kuwaza starehe za nje ya kiwanja ambazo hazina maana .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers