HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 May 2014

WAZEE 15 KUTIMULIWA CHELSEA !!!!

Klabu cha soka cha Chelsea kinatarajia kuwamwaga wachezaji Kumi na tano katika kikosi cha wachezaji wa kikosi cha kwanza katika wakati huu wa kiangazi .

Katika taarifa iliyoandikwa kutoka katika Mtandao wa Daily Express zimesema Mmiliki wa Le  Blues Roman Abramovich atamweleza kocha wa Timu hiyo  Mourinho kutengeneza kiksoi cha kushambulia zaidi na yupo tayari kumsaidia kifedha katika soko la kununua wachezaji .
Washambuliaji watatu  Fernando Torres, Demba Ba na  Samuel Eto'o wataondolewa. 

Majina mengine makubwa yanayotarajiwa kuondolewa katika timu hiyo kwa kuuzwa ili kuongeza pesa ni wafuatao David Luiz, Ramires, John Obi Mikel na Victor Moses.
Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Ashley Cole anatarajiwa kuondoka  Bure, Japokuwa mchezaji Mwezake Frank Lampard na  John Terry watabakia katika timu . 

Mchezaji aliye kwa mkopo kutoka Everton  Romelu Lukaku anataka kurudi  Chelsea lakini atauzwa  Tottenham ili kumsaidia  Mourinho kupata Pesa za kununua mshambuliaji mpya.

Wachezaji wengine ambao wataachwa ni  Marko Marin, Oriol Romeu, Gael Kakuta, Josh McEachran, Hilario na Sam Hutchinson.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers