Nahodha wa Timu ya Taifa ya Uingereza Steven Gerrard amestaafu kucheza soka ya Kimataifa baada ya kuitumia Uingereza mara 114.
Gerrard, 34, alicheza mechi yake ya kwanza mwaka 2000 na Kupata Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Ukrane Aliichezea Uingereza kwa mara ya Mara Mwisho mwaka 2014 kwenye Kombe la Dunia na kupata Suluhu ya
0-0 Dhidi ya Costa Rica.
"Nimefurahia kila dakika ya Kuiwakilisha Nchi Yangu .Ni siku ya Huzuni kwangu ," Kiungo huyo wa Wa Liverpool amesema ".
Gerrard sasa atakuwa anabeba majukumu ya kuwa Balozi wa chama cha soka cha Uingereza kimataifa .
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ameifungia Timu yake mabao 21wakati alipoiwakilisha timu yake ya taifa katika mashindano sita tofauti .
"Ulikuwa Uamuzi mgumu sana kuufanya. Ni jambo ambalo nilikuwa nikilitafakari kwa Muda Kidogo, sio mara baada ya kombe la Dunia kumalizika ,"Kiungo huyo wa Liverpool amesema .
"Nilitaka shauri mbalimbali kutoka kwa watu wangu wa karibu -Wachezaji ambao ninacheza nao , Wachezaji wa zamani ambao nilicheza nao zamani , Makocha ambao nilikuwa nao miaka kadhaa iliyopita .
"Huu umekuwa uamuzi mgumu sana, Ni moja kati ya maamzuzi magumu ambayo nimewahi kuyafanya Tangu nilipotimu miaka 18 na kuwa Mchezaji wa kulipwa ."
Gerrard ataendelea kuitumiakia klabu yake Liverpool, ambayo ndiyo alinaza nayo kuchezea mwaka 1998 Dhidi ya Blackburn Rovers.
Mwandishi mwandamizi wa BBC michezo Phil McNulty anasema :
"Gerrard alivunjwa moyo Baada kutolewa kwa uingereza katika mechi michuano ya kombe la Dunia na sasa hatokuwemo katika michuano ya ulaya ya mwaka 2016 itakayofanyika Ufaransa .
"Kwa uwezo mkubwa alionao ,Amesikitishwa na matokeo waliyoyapata Nchini Brazil na ilikuwa wazi kuwa kijana 34-na aliona kuwa uwezo wake ulikuwa unampa mkono wa kwaheri ."
No comments:
Post a Comment