HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 July 2014

NYERERE"BADO MIAKA 130 TANZANIA KUTWAA KOMBE LA DUNIA "


Kitwana Manara, Omar Gumbo, Jamal Rwambow, Hassan Mnyenye, Godfrey Lutego, Sunday Manara, Abdala Kibadeni, Abdala Maulid, Idd Azan, Adolf Rishard, Lawrence Mwalusako, Sekilojo Mambua, Madaraka Seleman, Moh'd Hussein, David Mwakalebela and Moh'd
Mwaka 2014 Ujerumani imetwaa Ubingwa wa  Dunia katika Ardhi ya America ya Kusini ni kwa miaka zaidi ya Sabini na Minne wameweza kuvunja Rekodi hiyo na kwa wasiyojua Historia Mjerumani Ndiye aliyetawala zaidi  Tanganyika ambayo sasa inaitwa Tanzania lakini kabla ya majina yote hayo Tanzania ilikuwa ikiitwaa Deutsostafrika yaani  Dola ya Kijerumani afrika mashariki wanaojua Historia watakuwa wanajaribu kunielewa.
Nchi ambayo nimekutajia ilipata kuwa na kiongozi mmoja makini na Mjanja sana Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye mimi kila napomkumbuka Mzee huyu nakumbuka majina kama Mwitongo,Burito kwa wenyeji wa Mkoa wa mara mtakuwa mnajua maana ya Majina hayo na maana yake , Mzee huyu aliwahi kunukuliwa akisema hivi “Itachukua Miaka mia moja na Themanini Mtanzania wa kawaida kuwa sawa na Mjerumani “.
Watu walilitazama jambo kama mzaha na wengine wakisema Mzee Yule ni muongo lakini mimi nina ungana nae na kuongeza kuwa Imebaki miaka mia moja thelathini Tanzania itwae Ubingwa wa Dunia hii ukianzia Tangu tulipopata uhuru December 9/61 mpka leo sababu tumeshekherea miaka hamsini ya Uhuru na Bado hatuja waweza kucheza robo fainali ya Mataifa ya afrika ,Na Mfano mzuri ni kuwa mara ya kwanza Tanzania ilikuwa inacheza Bila jezi hiyo ilikuwa miaka ya Nyuma .
Kuna mambo mengi ambayo Tanzania hayaja kaa sawa mpaka Muda huu kama Elimu,Afya,Miundo Mbinu ,Na la mwisho ambalo ndilo hatuna kabisa ustaarabu mambo haya Mjerumani anayo Kabla kombe la Dunia Halijaaanzishwa sisi Mambo hayo mpaka leo Bado hatuna au Tunafanya Kinyume.
Kwa Mfano Elimu Anayepata Divisheni 4 anakuwa mwalimu anaenda kuwafundisha kufeli wanafunzi wengine kwa hiyo tunazidi kuongeza wajinga kila sehemu tunakuwa na wanamichezo wajinga wasioelewa namna ya kujilinda kimichezo wasiofundishika na  ukiwaletea kocha mzungu ndio kabisa maana wa Kiswahili tu hawamwelewi! Na Walio wengi ambao wamepata Idea ya kusoma na wakaelewa wengi wao wapo Dar Es salaam .
Lakini huko mikoani kwenye Vipaji  Vingi zaidi kuna mamia ya mambumbu wasio jua lolote kwa sababu hata mwalimu ukimpangia shule mkoani haendi kisa hajaingiziwa Pesa na miundo Mbinu mibovu je mpaka mambo haya yakae sawa  ujerumani itakuwa ishatwaa Ubingwa mara Ishirini na Tano Brazil Arobaini Tanzania inaweza kuwa imshafuzu labda mara nane kucheza kombe la Dunia tena Bila kushinda mechi yoyote kwenye makundi lakini kwa hari ilivyo inaonekana kadri ujerumani inavyozidi kuendelea Ndivyo Tanzania inavyozidi kuwa maskini Je unadhani kuna maendeleo ya soka kweli ?
Mpaka sasa kuna wachezaji kama Haruna Moshi, Shomari Kapombe , Mrisho Ngasa ambao wameshawahi kwenda ulaya kujaribu kucheza soka na wamechemka lakini kuna wakenya ambao wanaongezeka Tanzania na wanazidi kwenda ulaya na wanazidi kutwaa medali kadhaa katika mashindano ya kimataifa hii ina maana mwalimu Nyerere alishajionea haya miaka iliyopita je tangu amefariki kipi tumefanikiwa mpaka sasa kama wajinga wanazidi kuongezeka miundo mbinu haija kaa sawa Je nasema Uongo kuwa Nyerere Hakukosea !  
Hivi Ni kipi ambacho hasa tunajvunia katika michezo ukitazama Zimebaki Story aah Mwaka Themanini Tulifuzu mataifa ya Afrika Nigeria ,Aaah Nyambui Alileta Medali Madola na Filbert Bayi alileta Medali Na hata ilifika fainali kombe la Shirkisho baada ya hapo Rais Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akasema Tanzania Itaendelea kuwa Kichwa cha Mwendawazimu anaejiskia Kunyoa Basi ananyoa na Ndio Kauli Pekee ambayo Tanzania Tunaweweseka nayo kwani Mzee mwinyi aliitoa kwa Uchungu sana na ilitoka Moyoni kisa tulifungwa Mbele yake kwa sababu tu kuna Baadhi ya wachezaji inasemekana walifungisha Je? wachezaji hao walikuwa na Elimu ya Kutosha jibu hawakuwa nayo wangekuwa nayo wasingekubari.
Kwa hiyo bado miaka Mia Moja na Thelathini kwa Tanzania Kuchukua Kombe la Dunia ..

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers