HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 July 2014

RAIS KIKWETE ,JUMUIYA YA MADOLA NA MICHEZO YOTE WAMEKUDANGANYA MCHANA KWEUPE!Rais wangu, Jemedari wangu na Amiri Jeshi mkuu wa Nchi yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Vyama vya Michezo na Wizara ya Michezo Imekudanganya na kukufanya wewe kama Babu yao.

Rais Tangu uingie Madarakani  Mwaka 2005 umekutana na Viongozi wa  Vyama Mbalimbali vya michezo kwa Bahati Mbaya hakuna kiongozi hata mmoja aliyekueleza ukweli, wengi wao waliomba kitu ambacho sio sahihi pengine walikuwa wanakuogopa lakini naweza sema hawajui kutumia nafasi Adhimu ya Kukutana na wewe uso uso! 

Watu waliokudanya Zaidi hivi karibuni ni wanamichezo waliokwenda kushiriki Jumuiya ya Madola pale Glascow Uskochi hawa walikuwa wanalia kwa Muda Mrefu sana maandalizi ,Maandalizi Mzee wangu Ukasema isiwe Tabu ukawapeleka Kambi Nje wakaa kwa Muda walioona unafaa, Binafsi yangu niliona kuwa hakuna cha timu pale! ni ubabaishaji mtupu hayo yaliwahi kufanywa hata na Rafiki yako Maximo kuipeleka Stars Brazil .

Timu hii ya Jumuiya ya Madola ambayo inawachezaji wa Riadha,Ngumi,Judo ,Kuogelea,  kwangu mimi hakuna Tofauti na kikosi cha mastaa wa Real Madrid wanaokuja Kutariii na sio kucheza soka Zidane,Figo,Salgado Hawaji kucheza mpira wanakuja kutarii .
Hivi Rais wangu wanakuja na dawa za kukufanya uingine mkenge au?  maana wanakudharirisha tu hawa 
Ningekuwa mimi Ndio napata Bahati ya Kukutana nawewe uso kwa uso ningeomba yafutayao kwako katika michezo.

Kwanza kabisa ningekuomba ujenge shule tano  kuu za michezo tofauti ukiziweka katika Kanda tofauti shule ya Riadha Arusha ,soka Dar es salaam na Zanzibar ,Masumbwi Musoma,kuogelea mikoa kanda ya Ziwa   pamoja na Pwani ,kwanini nasema hivi Sisi shida yetu ni Maandalizi ya awali sio kuchukua watu ambao wamekwisha komaa ndo kuwapeleka Uskochi  wamekwenda kutarii Mh Rais kwa utaratibu tulionayo sasa sidhani kama tutafanikiwa kama ulivyowahi kusema wewe mwenyewe wakati ukipokea ujio wa Kombe la Dunia "Mpaka Mwisho Dunia hatutofanikiwa ni kwa mambo kama haya hawakuelezi ukweli !

Mimi nakueleza Rais wangu Inawezekana aliyetuloga katangulia mbele ya haki sababu haiwezekani tunachemka kila siku halafu tunakaa na kubandika kwenye magali yetu Picha za Usain Bolt,Beckham,Causic Clay Mohammed Ally .

Mbona hakuna Picha za Nyambui,au Ikangaa kwa sababu hakuna shule za michezo na hakuna anayewajua  wachezaji tuliopeleka wanatakiwa kuwa makocha na sio wachezaji Mh rais nahuzinika kuwa utakapotoka madarakani utoka kama kaka yako Mkapa Bila kumtunza mwanamichezo yoyote aliyeleta Medali katika michezo ya kimataifa sizungumzii waliofanya vizuri kwenye klabu au timu za nchi Nyingine wakati mwingine huwa najiuliza Hivi ni Laana au Tumelogwa tu Mkuu mbona wanakufedhehesha Kila siku wanasema hoo hari ya Hewa hivi hiyo hewa wanayosema mbona kenya ,Uganda,Ethiopia Nigeria Ghana haziwaathiri au wenzetu wanavuta hewa Tofauti na tunayovuta sisi .

Rais Kikwete hawa Vijana wanakuhujumu Mimi nakuhakikishia kama hatutajenga shule za michezo zenye ubora wa Kimataifa na kuweka Viongozi sahihi hatutofanikiwa mpaka Yesu ninae mwanimini au Isah Bin Mariam unavyomwita wewe atakaporudi Tena kuchukua watu wake na hata kama hakasamehe Dhambi tulizofanya akaamua kuchukua watu kwa Medali walizoshinda kwenye michuano Mbalimbali bado tutashindwa kwenda Mbiguni . Kikwete umehujumiwa na Tasnia ya wanamichezo wanao Taka mafanikio Bila kufa .
Kazi unayo Mkuu wangu wa Nchi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers