HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 July 2014

TAMBUENI THAMANI YA UAKILISHI WENU JUMUIYA YA MADOLA(KIKWETE)

ta6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi ya kukabidhi bendera iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.

Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzanai Jakaya Mrisho Kikwete hii leo amekutana na wachezaji wa timu ya taifa ambao watakwenda mjini Glasgow nchini Scotland kushitriki michuano ya jumuia ya Madola ambayo imepangwa kuanza July 23-August 03 mwaka huu.

Raisi kikwete amekutana na wachezaji hao jijini Dar es salaam na kuwahusia suala la kujituma wakati watakapokuwa kwenye michuano hiyo ambayo hushirikisha nchi mbali mbali duniani kote.

Kikwete amewataka wachezaji wa Tanzania kutambua thamani waliyopewa ya kwenda kuiwakisha nchi kwenye michuano hiyo, hivyo amewasisitiza suala la kutambua umuhimu wa kiu ya mashabiki pamoja na wadau wa michezo nchinia mbao kwa miaka mingi iliyopita wamekua na hamu ya kuona angalau ushindi wa medali moja ya dhahabu unapatikana.

Naye katibu mkuu wa kamati ya Olympic Tanzania Filbert Bayi ameishukuru serikali ya aawamu ya nne kwa mchango mkubwa iloiyoutoa kwa mwaka huu katika maandalizi ya timu ya taifa kwa kukamilisha mpango wa kambi ya nje ya nchi.

Bayi amesema anaamini huo ni mwanzo ambao unatoa mwanga kwa taifa la Tanzania ambalo lina hamu ya kurejesha heshima yake katika Nyanja ya michezo duniani.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers