HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 July 2014

NOIJ STARS ITACHEZA KIUMOJA ZAIDI(SIKILIZA ALICHOSEMA )
Kocha Mkuu wa Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Mart Noij amesema timu yake itacheza kwa umoja ilikuhakikisha inapata ushindi katika Mchezo wa  kutafuta Timu itakayoingia kucheza kwenye Makundi ambayo yatatumika kufuzu fainaliza Kombe la Mataifa ya afrika huko Morocco ambapo stars itakuwa inakipiga Dhidi ya Msumbiji siku ya jumapili katika uwanja wa taifa jiji Dar Es Salaam.
  
SIKILIZIA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI  Kikosi cha Stars, ambacho kilikuwa Kambini huko Botswana kwa Wiki mbili na kisha kwenda Mbeya, kimeimarika kwa kuwapata Maprofeshenali wake Watatu ambao ni Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wa Klabu ya TP Mazembe ya Congo DR na Mwinyi Kazimoto anaechezea Klabu ya Al Markhiya ya Qatar.

Kwenye Raundi iliyopita, Taifa Stars iliibwaga Zimbabwe kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza Bao 1-0 Jijini Dar es Salaam na kutoka 2-2 huko Harare.
Mshindi wa Mechi kati ya Taifa Stars na Msumbiji ataingia Kundi F ambalo lina Timu za Zambia, Cape Verde na Niger.


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers