Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya (shoto) akitangaza viwango vipya vya mishahara kwa kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Viwango hivyo vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi vinazigusa sekta za Afya,Huduma za Kilimo, Viwanda na Biashara, Mawasiliano, Sekta ya Madini, Bandari na sekta ya Uvuvi, Wafanyakazi wa majumbani,sekta ya ulinzi Binafsi na Hoteli. Habari na Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Ufafanuzi wa viwango hivyo.
1. Huduma za Afya - Tshs 80,000/=
2.Sekta ya Kilimo - Tshs 70,000/=
3.Viwanda na Biashara - Tsh. 80,000/=
4. Usafirishaji na Mawasiliano
-Huduma za anga 350,000/=
- Clearing and Fowarding 230,000/=
- Mawasiliano ya Simu 300,000/=
- Usafiri wa nchi kavu 150,000/=
5.Madini - Migodini 350,000/=
- Wachimbaji wadogo -150,000/=
- Wauzaji wadogo na watoa leseni 250,000/=
- Brokers Licenses 150,000/=
6. Maji (Bahari na Uvuvi) - Tsh. 165,000/=
7.Majumbani:
- Majumbani (mabalozi na wafanyabiashara wakubwa)- isiwe chini ya Tsh 90,000/=
- Maafisa wenye sitahili ya kulipiwa huduma hii -isiwe chini ya Tsh.80,000/=
- Wengineo - Tshs 65,000/=
Mahotelini:
- Hoteli kubwa za kitalii - 150,000/=
- Hoteli za kati - 100,000/=
- Hoteli ndogondogo,mabaa, nyumba za wageni na migahawa- 80,000/=
8. Ulinzi Binafsi.
-Makampuni makubwa na makampuni ya kigeni - 105,000/= - Makampuni mengineyo- 80,000/=
9. Sekta nyingine ambazo hazikutajwa - 80,000/=
kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment