Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki
hazitauzwa tena kwenye magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye
mtandao au kwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.
Kesho (Novemba 8 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo
Shooting wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal
Union. Jumapili ni mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa
Taifa ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya
rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Mechi za Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya
Stand United na Mbeya City (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na
Kagera Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili
kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda
kutoka Mtwara.
No comments:
Post a Comment