HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 August 2010

VODACOM IMEKABIDHI VIFAA VYA VILABU VYA LIGI KUU

Vodacom Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 290 kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa mwaka 2010/11. Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza alisema ni matumaini ya kampuni yake kwamba vifaa hivyo vitakuwa ni kichocheo cha kuinua kiwango cha soka hapa nchini. Amesema huu ni msimu wa tisa tangu Vodacom ianze kudhamini Ligi hiyo na kwamba Vodacom inafarijika kuona kiwango cha soka kikipanda.
Mbali na kukabidhi zawadi hizo, alivishauri vilabu kutafuta njia nyingine za kuongeza mapato ikiwamo kutafuta wadhamini wengine ili kukabiliana na kupanda mara kwa mara kwa gharama za uendeshaji wa vilabu. Alisema msimu huu Vodacom imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kudhamini ligi hiyo. Alisema kati ya hizo shilingi milioni 667 zimetengwa kwa shughuli za uendeshaji wa Ligi ikiwemo nauli za timu pamoja na gharama nyingine kama posho za marefa. Rwehumbiza alisema msimu huu vifaa vimeboreshwa zaidi na kuvitaka vilabu kuvitumia vifaa hivyo kuboresha Ligi. Alivipongeza Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya vizuri msimu uliopita na kuvitakia kila lakheri msimu huu. Aidha Mkuu wa Udhamini huyo alitoa rai kwa vilabu kuvitumia vifaa hivyo kama changamoto ya kufanya vizuri katika Ligi ya Vodacom msimu wa mwaka 2010/11na hivyo kutupatia mwakilishi bora wa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers