Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar Mecky wakati akiongea na waandishi wa habari |
Nusu fainali zitapigwa Uwanja wa Taifa kesho Jumatano, ambako Simbaa itavaana na Azam huku Mtibwa sugar ikipepetana na Jamhuri. Mchezo wa kwanza utaanza saa nane mchana wataanza Mtibwa sugar na Jamhuri ya Zanzibar na mchezo wa pili ni kati ya Simba Vs Azam utakao anza saa kumi.
MTIBWA, Simba, Azam FC na Jamhuri ya Pemba zimefanikiwa kupenya hatua ya nusu fainali ya michuano ya BancABC SUP8R inayondelea katika vituo vinne hapa nchini.
Michuano hiyo inayodhaminiwa na Banc ABC, ilikuwa ikirindima katika
miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar na sasa imefikia
hatua ya nusu fainali.
August 12 mwaka huu kwenye dimba la Chamazi, Mbagala jijini Dar es
Salaam, ilishuhudiwa kwa mara ya pili nyuki wakikatiza uwanjani hapo,
Jamhuri iliichapa Mtende kwa mabao 4-0.
Mabao ya washindi yalifungwa na Sadik Rajab dakika ya 28 na 45,
Selemani Nuhu dakika ya 82 huku Suleiman Ally akikandamiza la nne
dakika ya 90.
Kwenye dimba la Kirumba Mwanza, makinda wa Simba waliibuka na
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto yote yakitiwa kimiani na Edward
Christopher, wakati huko Moshi kwenye Uwanja wa Ushirika, Azam FC
iliifunga Polisi Morogoro kwa mabao 2-1.
Bingwa katika michuano hiyo atajitwalia kombe na kitita cha sh
milioni 40, wa pili milioni 20 huku timu zitakazoishia nusu fainali
kila moja itapata sh mil 15 na zitakazosalia zitajipoza kwa sh milioni 5
kila moja.
No comments:
Post a Comment