YANGA SC leo imetoka nyuma kwa mabao
2-0 na kushinda 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga itemize
pointi 14, baada ya kucheza mechi nane, hivyo kujiweka sawa katika nafasi ya
tatu, ikizidwa pointi tatu na Azam inayoshika nafasi ya pili na pointi nne na
Simba inayoongoza ligi hiyo.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa
zimekwishafungana mabao 2-2, Ruvu Shooting wakitangulia na baadaye Yanga
kusawazisha.
Mabao ya Ruvu yalifungwa na
mshambuliaji Seif Abdallah dakika ya tatu na lingine dakika ya 10, yote
kutokana na mipira kutoka upande wa kulia mwa Uwanja, la kwanza mpira wa adhabu
na la pili krosi.
Rashid Gumbo aliangushwa nje kidogo
ya eneo la hatari na Mbuyu Twite akaenda kupiga mpira wa adhabu uliotinga moja
kwa moja nyavuni dakika ya 20 na haraka haraka Jerry Tegete akauchukua mpira
kwenye nyavu za Ruvu na kwenda kuuweka katikati.
pallanyor.blogpcha
Jeryson Tegete akishangilia bao alilofunga |
Hilo lilikuwa bao la pili Twite
anaifungia Yanga kwenye ligi, ndani ya mechi nane alizocheza.
Kipindi cha pili Yanga walirudi na
kasi tena na kufanikiwa kupata bao la ushindi dakika ya 65, ambalo lilifungwa
na Kavumbangu.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo
kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Coastal Union iliifunga Mtibwa Sugar mabao
3-1 mabao ya Juma Jabu, Daniel Lyanga na Lameck Dayton, la Mtibwa lilifungwa na
Shaaban Nditi.
No comments:
Post a Comment