Bingwa wa michuano ya
BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es
Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni 40 wakati makamu bingwa
sh. milioni 20. Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja
itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
Timu zimepangwa
katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba (mabingwa wa
Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi ni Super
Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zote za
Tanzania Bara.
Mechi za ufunguzi
keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto
vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na Super Falcon vs
Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini
yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi
itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote
zitachezwa Dar es Salaam
Mdhamini bancABC
atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine,
malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake
imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya
Vodacom.
No comments:
Post a Comment