Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini yapauni za
Uingereza 45,000 sawa na dola za
kimarekani $71,000 na chama cha mpira
cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kuhusu
beki wa Chelsea Ashley Cole.
Halmashauri huru imempata na hatia kwa
kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha ukoo na kabila la
mpinzani kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na
ndani mzungu.
Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki.
.Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter yalitokea baada ya
Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo wake Rio aliyedai
kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment