Timu ya vijana ya kuogelea
kutoka Tanzania imefanya vizuri katika mashindano yaliyoshirikisha timu 20
kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na mashindano hayo kufanyika jijini
Nairobi kuanzia tarehe 17 hadi 19 May 2013 katika shule ya Aga Khan. Washiriki
wa mashindano hayo walitoka katika nchi za Tanzania, Kenya, na Uganda ambazo
kila mmoja alitaka kumshinda mwenzake.
Wasichana kutoka Tanzania wamekuwa
washindi wa kwanza kwa kupata alama176 points dhidi ya timu 24. Timu ya Uganda
Dolphins imeshika nafasi ya pili kwa
kupata alama 148 ambao walijaribu kuonyesha upinzani kwa timu yetu. Timu ya
Tanzania kwa upande wa wanaume imeshika nafasi ya 6 dhidi ya timu za wanaume 19
zilizoshiriki katika mashindano hayo. Hii ilisababishwa na ukweli hatukwenda na
wachezaji wa kutosha kiasi hawakuweza kushiriki katika relay na tulipata alama
54. Matokeo ya jumla ni kuwa Tanzania tumekuwa watatu kwa kupata alama 230
ambapo Dolphins Uganda wamekuwa wa kwanza kwa kupata alama 278 na Makini ya
Kenya wapili kwa kupata alama 240.50.
Waogeleaji
wetu
walikuwa na ari ya juu licha ya hofu tulikuwa nayo hapo kabla ya baridi
kali na
tunamshukuru Mwenyezi Mungu hakukuwa na baridi kali labda wakati wa
usiku.
Muda
wote wa mashindano waogeleaji wetu wakati wanapiga mbizi walishangiliwa
kwa
sauti ya juu na shukrani kwa wazazi ambao muda wote walikuwa
wanashangilia ``Tanzania
oye``. Kwa hakika ni matokeo ya kufurahisha licha ya medali, wachezaji
wetu waliweza kushusha muda wao na kuweka muda mpya(PB)na
wengine wameteremsha muda wao hadi sekunde 10. Waogeleaji wetu walikuwa
walikuwa katika kiwango bora kuanzia siku ya mwanzo ya mashindano
walipoanza
kuogelea mita 100 (IM) muogeleaji
anaogelea stroke zote 4. (25m butterfly, 25m backstroke, 25m breastroke and 25m
freestyle).
Kila aliyeshiriki
alikuwa anajaribu kumshinda mpinzani wake na kwa kweli tulikuwa na ushindani
mkali kutoka kwa waganda na wakenya . Muogeleaji Sonia Tumiotto (KAPTENI WA TIMU) alipata
dhahabu na kuweka rekodi ya mashindano kwa wasichana miaka 11 mita 100 IM kwa
kuogelea muda mpya wa dakika 1:18:70. Medali ya silver ilienda kwa Smriti Gokarn ambaye alikuwa na upinzani mkali
kutoka kwa wasichana wenzake miaka 10 na kuogelea muda wa dakika 1.25.54
Siku ya pili ya
mashindano hayo waogeaji wetu waliweza kupata mbalimbali wakiwemo. Selina
Itatiro (silver, miaka 9 wasichana, 25m fly), Tessa Francis (bronze, miaka 9
wasichana 25m fly, na silver 25m free), Smriti Gokarn (silver, 50m fly. Silver
50m breast, dhahabu 50m back, silver 25 free), Sonia Tumiotto(11) (Dhahabu, 50m
fly, dhahabu 50m breast, dhahabu 50 back, dhahabu 25 free), Amani Doggart
(bronze miaka 8 wasichana 25m breast) ,Njukia kihara (silver, miaka 7 breast),
Dhashraad Magevaran (10)(bronze, 50m back).
Waogeleaji wetu pia
wamekuwa washindi na kupewa zawadi ya vikombe kwa kila umri. Waliopata vikombe
kwa wasichana miaka 8 ni Amani Doggart nafasi ya tatu, Tessa Francis miaka 9 wasichana
nafasi ya tatu, Smriti Gokarn miaka 10 nafasi ya pili na kuweka rekodi mbili na
Sonia Tumiotto miaka 11 wasichana nafasi ya kwanza na kuweka rekodi 3.
Siku ya jumapili
ilikuwa ndio siku muhimu na ya kweli kwa Tanzania ambapo waogeleaji wa relay
waliweza kupata dhahabu kila tukio tuliloshiriki. Katika miaka 8 wasichana kwa
timu ya relay iliyowashirikisha Diya
Patel, Maia Tumiotto, Ursula Khimji and Amani Doggart walipata dhahabu mbili
kwa medley relay(KILA MUOGELEAJI
ANAOGELEA AINA MOJA YA MTINDO WA KUOGELEA) na freestyle relays,
wasishana wa miaka 11 yenye waogeleaji Sonia
Tumioto, Selina Mehta, Maya Kihara, Tallin Stengell nao waliweza
kuchukua
medali mbili za dhahabu kwa medley relay na freestyle relays. Miaka 10
wavulana kwa tim u yenye waogeleaji Dhashraad Magesvaran, Urav Shah,
Alexander
Belikov and Vansh Ladwa nao walichukua dhahabu katika mtindo wa medley
relay and freestlye relays. Juhudi za pamoja kati ya
wasichana na wavulana ndizo zilizotuwezesha Tanzania kuwa nafasi ya tatu
kwa matokeo ya jumla kwa mwaka 2013
Naye kocha wa timu
hiyo Mohamed Abdulazizi alisema kuwa “Tuliwaandaa wachezaji kimwili na kiakili
kuweza kukabiliana na lolote litakalojitokeza mbele yetu ndio siri ya mafanikio
haya ya kufurahisha.
Tanzania
iliwakilishwa na Sonia Tumiotto (Team captain), Harry McIntosh (vice captain), Dashraad
Magesvaran (boys captain), Smriti
Gokarn (girls captain), Reuben Monyo, Njukia
Kihara, Prashraad Magesvaran, Oliver McIntosh, Shiv Shreekumar, Gian Maria, Vansh
Ladwa, Alexander
Belikov, Urav Shah, Maia Tumiotto, Diya Patel, Amani Doggart, Celina Itatiro,
Tessa Francis, Janice Njuguna, Selina Mehta, Maya Kihara, Mariana Pipollo, Piya
Shah, Talin Stengel and Ursula Khimji. Makocha wengine wqa timu hiyo ya waogeleaji
25 walikuwa ni Kocha Alex Mwaipasi na Kocha Kanis Mabena na Mkuu wa msafara
alikuwa ni Inviolata Rwelamira Itatiro.
Tunajivunia vijana
hawa kwa kutuwakilisha vyema na kufanya Tanzania kungára, Hongera sana pamoja na wazazi wote. Hii ni mara ya pili
katika historia ya mchezo wa kuogelea ambapo timu ya vijana imeweza kwenda
kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki na kurudi na vikombe na medali nyingi.
Mara ya kwanza ilikuwa timu ya vijana pia ilipoweza kurudi kwa kikombe cha
mshindi wa pili baada ya kujikusanyia medali 76 ambapo mashindano hayo
yalifanyika Kampala mwezi wa 10 tarehe 22 na 23 mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment