Wanamichezo watano waliohudhuria miechezo ya Olympic
jijini London Uingereza kutoka nchini Cameroon, wanasema wanataka
ukimbizi kuendelea kubaki nchi Uingereza baada ya kutoweka katika kijiji
cha Olympic wiki iliyopita.
Wanamichezo hao wanaume watano wote wakiwa ni
mabondia wameiambia BBC kuwa waliondoka katika kijiji cha mashindano ya
Olympic mashariki mwa London baada ya kutishiwa na maafisa wa juu wa
timu ya Olympic ya Camerron, kuwa wangeadhibiwa iwapo wangeshindwa
katika mashindano hayo.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake mmoja wa mabondia hao amesema wanataka kubaki
nchini Uingereza ili kuendeleza taaluma yao ya kimichezo katika ndondi.
Hata hivyo mkuu wa msafara wa timu ya
wanamichezo wa Cameroon David Ojong, amesema mabondia hao wamedanganya
na kuwa hakuna yeyote aliyewatishia.
Amesema mabondia wote walipata mafunzo ya kutosha pamoja na kulipwa vizuri na sababu hiyo huenda ni kuhalalisha kurotoka kwao.
Mmoja wa mabondia hao Thomas Essomba amesema
viongozi wa msafara wao waliwatisha kwa kuanza kuwaamuru wale waliokuwa
tayari wameshiriki michezo mingine na kushindwa kusalimisha hati zao za
kusafiria.
Naye bondia mwingine Blaise Yepmouo, amesema kamwe hawataki kurejea nchini mwao kwani taaluma yao ya kimichezo itakufa.
''Tunataka kuwa mabondia wa kulipwa na hatuwezi
kurudi Camroon.'' Anasema. ''Na hata ikiwa tutarudi hatuwezi tena
kuendelea na ngumi. Watano waliopo hapa wanataka kuwa mabondia wa
kulipwa na ndiyo maana tunaomba udhamini.''
Wamesema kuwa kubaki kwao Uingereza kutawawezesha kupata udhamini na hivyo kuendeleza vipaji vyao katika mchezo huo. BBCSWAHILI YATHIBITISHA
No comments:
Post a Comment