Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen leo (Agosti 1 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 21
kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu. Wachezaji walioitwa
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti
kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni
tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata. Makipa walioitwa
kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba)
na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd
(Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam),
Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba),
Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Wachezaji wanaounda
safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
No comments:
Post a Comment