MAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII WANAPOTIWA HATIANI NA WENYE MALI
|
Hizi ni moja kati ya kazi za wasaniii zilikamtwa kwenye msako wa wanao tengeneza fialamu feki |
MSANII WWA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM
Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki ambapo walikamatwa kwa kushilikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es salaam picha na
|
MSANII MOHAMED
NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA
WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA
JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI.
KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi
za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za
wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa
wasanii wanaotoa kazi hizo
Msemaji wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa
ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii
wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao
zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa
tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili
iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo
Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo
iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii
Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani
katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na dvd ndio inakuwa
imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa
masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao
bila kushiriki chochote
Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja
na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni
Mwapagata (
Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles
Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana
pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na
kuiomba serekali kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama
hizo zilizokamatwa
|
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment