Aliyevalia jezi nambari nne ni mchezaji mpya wa dar es salaam yanga afrika Mbuyu Twite akiwa ameveshwa jezi namba 4 ikiwa imeandikwa kwa Dhihaka jina moja la mwenyekiti wa klabu ya simba ya jijini DSM |
Mlinzi mpya wa klabu ya soka Yanga, Mbuyu Twite amewasiri leo jijini Dar es salaam na kulakiwa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo katika uwanja wa Ndege wa JKN ambapo baadaye alipakiwa kwenye gari maalum kulekea makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Aidha hakukuwa na kiongozi yeyote au mashabiki wa Simba wala askari aliyejaribu kumkamata kama ilivyokuwa kumetolewa Taarifa la kutaka kumkamata mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda, ambaye ana asili ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa wangemkata kwa tuhuma za kujipatia fedha kinyume na utaratibu dola za Kimarekani 30,000,
kabla ya kusaini Yanga, Twite alikuwa akitumikia klabu ya APR ya Rwanda alisaini Simba
na kuchukua dola 30,000.
, baadaye mchezaji huyo alibadili maamuzi na kutia saini kandarasi ya kuhudumu klabu ya Yanga na kurudisha
fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, timu hizo
zilikuwa zinammiliki mchezaji huyo kwa pamoja.
Twite
aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya
wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa
anakamilisha taratibu za kuhamisha familia yake .
No comments:
Post a Comment