Mbwana samata mchezaji wa Tp Mazembe ya DRC |
MABINGWA mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana wamefufua matumaini ya kutwaa ubigwa wa tano
wa michuano klabu bingwa afrika , baada ya kuifunga Zamalek ya Misri mabao 2-0 katika mchezo
wa Kundi B la Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa TPM, mjini
Lubumbashi.
,N. Kasongo alifunga bao la kwanza
dakika ya 70, akimalizia pasi ya D. Kanda na Mbwana Ally Samata aliyeongeza la
pili dakika ya 77, akiunganisha pasi Tressor Mabi Mputu.
Mazembe sasa imefikisha pointi nne, baada ya awali kufungwa
na Al Ahly ya Misri mjini Cairo 2-1 kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na
Berekum Chelsea ya Ghana nyumbani, Lubumbashi.
Mechi nyingine ya kundi hilo Ahly inayoongoza
Kundi hilo kwa alama sita, dhidi Chelsea ya pili yenye alama nne, mjini
Cairo itachezwa saa 5:00 usiku. Zamalek haina alama na inashika mkia.
No comments:
Post a Comment