Raisi wa
shiriksiho als oka nchini TFF Jamal Malinzi amesema suala la kurejesha ofisi za
shiriksiho hilo maeneo ya Karume jijini Dar es salaam kama walivyoshauriwa na
FIFA, huenda likachukua muda kutokana na ukarabati ambao unatakiwa kufanywa
kwenye ofisi hizo.
Malinzi
amesema haoni sababu ya kuharakisha kurejea katika ofisi za zamani za TFF, ili
hali FIFA walitoa ahadi ya kusaidia sehemu ya ukarabati wa ofisi hizo, hivyo
amewataka wadau wa soka kuwa na subra na jambo hilo japo kuna wengine
wanaendelea kulivalia njuga kwa sababu zao binafsi.
Amesema
anaamini wapo wanaotamani kuona ofisi za TFF zikirejea Karume kwa malengo
mazuri, na pia wapo baadhi ya wadau wa soka nchini ambao wanashinikiza kwa
minajili ya kutaka uongozi wake uonekane kama ulikurupuka kuzihamisha ofisi
hizo na kuzipeleka kwenye jingo la PPF Tower.
Wakati huo
huo Jamal Malinzi akazungumzia sakata la Frank Domayo kusajiliwa na Azam FC,
akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania huko mkoani Mbeya miezi sita
iliyopita, hatu ambayo ilimfanya kuunda kamati iliyokuwa inaongozwa na Wakili Wilson
Ogunde kuchunguza
kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina.
No comments:
Post a Comment