DAVID LUIZ |
David Luiz Ametia saini ya Kandarasi ya miaka mitano ya kuhudumu katika klabu ya chelsea usiku huu tovuti ya klabu hiyo imethibitisha. Mlinzi huyo wa Brazil amabaye hajaitumikia klabu hiyo zaidi ya miaka miwili katika miaka yake mitano na nusu aliyosaini alipojiunga na klabu hiyo tangu
2011. Lakini mabingwa wa ulaya waliamua kumtia kitanzini kwa kandarasi nyingine kijana huyo mwenye miaka 25 atahudumu katika klabu mpaka 2017 na klabu hiyo imethibitisha kuwa wamemsainisha tayari
Luiz ameimbia tovuti ya klabu hiyo , www.chelseafc.com:
" Nina furaha sana kusaini kandarasi mpya na Chelsea Ni klabu kubwa .ninatazamia kushinda mataji zaidi na klabu hiii, Ninataka kucheza kwa muda mrefu katika ngazi ya juu .Na hii ndio maana ya kuchezea Chelsea ninapenda kila kitu kuhusu hii klabu na hasa kwa mashabiki wa timu hii
,ambao walinikaribisha kwa moyo mmoja na wamenipa ushirikiano wa kutosha
No comments:
Post a Comment