HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 September 2012

MKASA WA VODACOM LIGI ZANTEL AFRICAN LYON WAZUA BARAA TAIFA


KLABU ya African Lyon ambayo mchana wa leo imeingia kandarasi ya udhamini na kampuni ya simu ya Zantel imezuiwa kuweka mabango yake kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wala kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wao, kampuni ya simu ya Zantel katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.
  kumekuwa na hari ya sintofahamu na kuvuka kwa kasheshe baina ya wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa, dhidi ya viongozi wa African Lyon.
  Kandarasi hiyo ya miaka mitatu na inatarajiwa kuanza kuutumikia katika mchezo wa leo wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, utakaonza saa 10:30 jioni.
Meneja Mkuu wa Lyon, Rahim ‘Zamunda’ Kangezi anashikiria  msimamo huo wa endapo kama watazuliwa kiwanjani au kuvaa jezi za mdhamini wao na kuweka mabango utaendelea, basi wao hawatacheza mechi hiyo.
“Katika maboresho ya mkataba wa udhaimini wa Ligi Kuu wa Vodacom, hili lilikwishazungumzwa na limerekebishwa kwamba klabu zitaruhusiwa kuingia mkataba na kampuni nyingine za simu.
leo katika kikao cha kabla ya mechi walipeleka jezi  na zikapitishwa, sasa iweje wanaambiwa hatuwezi kuvaa, wao hawakubali, kama hatuvai na hatuchezi,”anasema Zamunda.
Alipoulizwa  kuhusu kanuni zitawahukumu wasipocheza kwa kushushwa Daraja, Zamunda amesema hawagomei mechi, bali wanagoma kucheza kwa sababu ya kuzuiwa, hivyo haoni ni kiasi gani kanuni hiyo itawahukumu, zaidi wao watapambana kupata haki yao na sana mechi hiyo itachezwa siku nyingine, ambayo TFF watakuwa tayari kuiruhusu Lyon kuvaa jezi za mdhamini wao.
 mchana, wa leo Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Sajid Khan ametangaza kampuni yake kuingia mkataba wa miaka mitatu kuidhamini Lyon, mbele ya Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo katika hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro), Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers