Kaike siraju wa kwanza kulia |
Promota wa ngumi za kulipwa nchini KAIKE MFAUME SIRAJU
amewafanyia kitendo si cha kiungwana mabondia chipukizi Issa Omar na
Mwaite Juma kwa kuwapambanisha tarehe 15/7 /2012 kwa makubaliano ya
kuwalipa kama ilivyo kawaida na badala yake kutowalipa mabondia hao
chipukizi
.Tarehe25/06/2012
aliwasainisha mkataba mbele ya katibu mkuu wa ngumi za kulipwa Tanzania
Ibrahim kamwe kuwa Issa omar kucheza na Ramadhan kumbele kwa malipo
madogo ya 80,000/=(elfuthemenini), alikadhalika kwa mwaite juma kucheza
na Anthony Mathias. Vijana walicheza na hawakulipwa.baada ya pambano
alitoroka, Walipojaribu kumdai haki yao kwa siku zilizofuatia walipigwa kalenda na kuwatembezatembeza kwa usumbufu kwa kuwaambia wamfate mara mango garden asubuhi na kuwagandisha mpaka jioni na kuwaambia njooni kesho
magomeni saa tano vijana walifika saa tatu na kuganda mpaka saa tisa
walipompigia simu aliwaambia waachane nae wakati mwanzo alikuwa
anawaambia wamsubiri sasa anawaambia waachane nae na kuwatisha.
Vijana
waliripoti kwa katibu mkuu Ibrahim kamwe nae akampigia simu kaike,nae
kaike akakubali kuwalipa kupitia ibrahim hivyo wasimfatefate,matokeo
yake anamzungusha katibu mara hivi mara vile hadi mwisho anadiriki
kusema kwanza wale watoto tu wasituzingue inaonekana hana nia ya
kuwalipa vijana hao. Nikiwa kama kiongozi nikajaribu kumuelimisha kaike
kuwa umeingia mkataba na mabondia wa kuwalipa baada ya pambano hivyo
yakubidi kuwalipa ili wajitahidi kwa kujua wana ajira ya uhakika na
kujitahidi kwao ni manufaa yetu na taifa kiujumla, ukizingatia siku hiyo
ya mchezo yule bondia mwingine aliumia sana jicho na wazazi wake
kulalamika kwa uongozi tunachezesha mabondia bila ya kuwalipa na
hatuwajali wanapoumia.
Mambo
yanayofanywa na kaike si ya kiungwana ni kuwavunja moyo mabondia
mabondia chipukizi,kudumaza ngumi na kufanya mchezo wa ngumi uonekane ni
mchezo wa wahuni kwa vitendo vya kihuni kama hivi.Halafu wanamasumbwi ulalamika hatupati wafadhili wakati uaminifu haupo baina yetu wenyewe.
regards
ibrahim kamwe
+255 713 501991
+255 784 501991
+255 767 501991
No comments:
Post a Comment