Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatoa vifaa vyenye
thamani ya sh. milioni 7.3 kwa Hospitali ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambazo
ni asilimia 5 ya fedha zilizopatikana kwenye mechi ya Simba na Azam.
Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi
wa msimu mpya wa 2012/2013 ilichezwa juzi (Septemba 11 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 146, 640,000. Washabiki 26,001 walikata
tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-2.
Sekretarieti ya TFF inatarajia kukutana na uongozi wa Hospitali ya
Temeke wakati wowote kuanzia leo ili kujua mahitaji halisi kabla ya kufanya ununuzi
wa vifaa husika.
Mgawanyo wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia
18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 22,368,813.56, asilimia 5 ya
mchango wa kusaidia jamii (Hospitali ya Temeke) sh. 7,332,000, uwanja sh.
10,148,318.64, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
4,059,327.46, TFF sh. 10,148,318.46 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 5,074,159.32.
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,014,831.86, kila timu sh.
32,265,025.93, asilimia 10 ya gharama za mchezo sh. 10,148,318.64, nauli kwa
waamuzi na kamishna sh. 80,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi na kamishna
230,000, posho ya waamuzi 400,000, tiketi sh. 4,495,800, maandalizi ya uwanja
(pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi uwanjani sh. 2.350,000
na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000.000.
Mchango wa kusaidia jamii kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuzindua
msimu uliopita kati ya Yanga na Simba ulikuwa sh. 15,000,000 ambazo zilikwenda
Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kusaidia uchunguzi wa kansa ya
matiti kwa akina mama.
No comments:
Post a Comment