HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 September 2012

KAMATI YA UTENDAJI YAREKEBISHA KANUNI


 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam imepitisha marekebisho ya kanuni kwa ajili ya Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.
 
Marekebisho hayo yametokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano uliofuta Ligi ya Taifa. Hivi sasa kutakuwa na Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.
 
Kutokana na marekebisho hayo ya kanuni; Ligi ya Wilaya itaendeshwa na Vyama vya Mpira wa Miguu vya Wilaya (DFAs), Ligi ya Mkoa itaendeshwa na Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa (RFAs).
 
Mechi za mchujo (play offs) kutafuta timu zitakazopanda kwenda Ligi ya Mkoa zitaendeshwa na RFAs wakati play offs za kupanda Ligi Daraja la Kwanza zitakazohusisha mabingwa wa mikoa zitasimamiwa na TFF.
 
Ligi za madaraja yote zitachezwa mwaka mzima kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers