Uongozi wa Yanga umesema unatafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa wachezaji walio na mikataba na klabu hiyo, lakini ambao kocha Ernest Brandt amependekeza waachwe kwenye dirisha dogo la usajili Januari.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kuwa kwa sasa hawawezi kutangaza majina ya wachezaji hao lakini aliithibitisha kuwa tayari wamepokea majina yaliyopendekezwa na kocha wao.
"Kwa sasa tupo kwenye kikao, hili suala tutalitolea maelezo baadae ila kuna majina ambayo kocha ametupatia na tutawaacha kwenye dirisha dogo la usajili," .
kwa kuwa suala hilo si la kukurupuka kwa kuwa kati ya wachezaji hao waliopendekezwa na kocha kuachwa wengine bado wana mikataba na klabu hiyo hivyo ni lazima zipatikane fedha za kuwalipa kabla ya kuwatema kwenye timu hiyo.
"Hatuwezi kuvunja tu mkataba na mchezaji... kuna mambo ambayo ni lazima tuyaweke sawa ili kusiwe na upande utakaolalamika," amesema Mwalusako.
Alisema klabu inajipanga kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Bara na Yanga inataka kujenga kikosi kitakochoendeleza mafanikio waliyoyapata kwenye mzunguko wa kwanza.
Yanga imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ikiwa inaongoza kwa pointi tano juu ya Azam yenye 24 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 23.

No comments:
Post a Comment