Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini
(TPBC) inaipa shavu BFT kwa juhudi zake za kuendeleza ngumi za ridhaa hapa
nchini kama kichocheo cha maendeleo ya ngumi pamoja na michezo yote kwa ujumla.
TPBC inatambua ugumu wa maisha pamoja
na matatizo yaliyopo kupata wadhamini kwenye mchezo wa ngumi. Juhudi za BFT za
kuandaa mashindano ya nguni za ridhaa mwaka huu ni zenye mweleko mzuri kimaendeleo.
Sisi kama Kamisheni iliyopewa na
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jukumu la kusimamia ngumi za
kulipwa nchini tunatambua kuwa ngumi za ridhaa ni chemchem ya nguni za kulipwa
hivyo tupo tayari kushirikiana na BFT kufanikisha mashindandano haya.
TPBC imefarijika na juhudi za BFT
katika ushiriki wake kwenye mashindano ya Olympic yaliyomalizika hivi karibuni
nchini Uingereza. Juhudi zenu zimeitangaza vyema Tanzania na kuwapatia mabondia
wa Kitanzania nafasi ya kujulikana ulimwenguni.
Kushiriki katika mashindano ya Olympic
sio tu kupata medali bali pia ushiriki wenyewe unaitangaza nchi kama moja ya
mataifa yaliyo mstari wa mbele katika maendeleo ya michezo ulimwenguni.
Tunatoa pia pongezi kwa Kamati ya Olympic
ya taifa (TOC) na baraza la Michezo la taifa (BMT) kwa juhudi zake za
kuhakikisha kuwa kila mara Tanzania inakuwa moja ya nchi zinazoshiriki katika
mashindano ya Olympic.
Sisi tunashiriki katika mapambano
mbalimbali ya ngumi za kulipwa ulimwenguni tunajua faida za kujitangaza huku kwani
tunajulikana kwa juhudi hizi.
Tutatoa wito kwa wadau wa ngumi na
michezo yote Tanzania ikiwa ni pamoja na watu binafsi, makampuni mbalimbali
pamoja na na taasisi zisizo za kiserikali kuwasidiaBFT katika juhudi za
kuendesha mashindano haya yatakayoanza hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment