Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho la soka la Tanzania TFF Sunday Kayuni akitoa wosia kwa waamuzi kabla ya kuanza majukumu yao katika ligi kuu Tanzania Bara
MKURUGENZI
wa Ufundi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni amewaasa
waamuzi kutumia filimbi yao vizuri ili kutenda haki wanapo kuwa
uwanjani.
Kayuni aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya waamuzi wa daraja la
kwanza
kituo Dar es salaam inayofanyika Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2012/13.
Amesema waamuzi ni kiungo muhimu katika kuendeleza mpira nchini, endapo watakuwa mahakimu wazuri wakiwa uwanjani.
Amewataka waamuzi hao kuchezesha kwa kufuata sheria 17 za soka, ili waweze kusaidia
soka la Tanzania kusonga mbele.
Kayuni
amewatahadharisha kuwa wanapochezesha vibaya wanajiharibia wao wenyewe,
kwani mchezo wa soka una mashabiki wengine na unaonyeshwa karibu kila
sehemu kutokana na teknolojia kukua.
Hawa ni baadhi ya waamuzi kuwa wakiwa wanapasha moto mwili |
"Endapo mtarubuniwa na viongozi wa vyama vya soka FA wanapokwenda kuchezesha mtoe taarifa kwa maandishi
katika ofisi yangu itawashughulikie kulikoni waamuzi kuendelea kuumia au kuwa mbuzi wa kafara," alisema Kayuni.
Hata hivyo, alisema amekuwa akisikia malalamiko kwa pembeni, lakini hajafikishiwa kwake.
Alisema amepata taarifa kuwa wanapokwenda mikoani kuchezesha viongozi wa FA wanawashinikiza timu zao zishinde na
mnapoacha kutekeleza matakwa yao wanawanyima posho zao.
Jumla
ya waamuzi wapatao 190 kutoka mikoa yote wameudhuria semina na kufanya
mtihani ya utimamu wa mwili. Semina hii inaratajiwa kufungwa kesho
jioni.
ROCKERSPORTS UNDERSTAND
No comments:
Post a Comment