Shirikisho la soka Tanzania (TFF),limetoa ufafanuzi kuhusu utaratibu unaotumika kuhusu kumpata mchezaji wa klabu
ya soka ya Chelsea Adam Nditi ambaye ni Mzanzibar na Raia wa Tanzania
kama anaweza kuchezea timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ambapo walijaribu
kuwasiliana na klabu ya soka ya Chelsea ambako ndiko anaposukuma gozi katika
timu ya Vijana , ilikutazama uwezekano wa kumpata mchezaji huyo . lakini klabu ya
Chelsea iliijibu Tff kuwa lazima wawasiliane na klabu kwanza halafu ndio wapate
ruhusa ya kuwasiliana Mchezaji huyo , Afisa Habari wa Shirikisho la soka la Kandanda la
Tanzania, Boniface Wambura amesema nia ya kumhitaji mchezaji huyo ni kutaka
akutane na kocha kwanza iliwafahamu kama yeye mwenyewe anataka kuchezea timu ya
taifa ya Tanzania au Vinginevyo kwani wanahofia kuwa wanaweza kumuita lakini
tayari akawa hana mwamko wa kucheza timu ya taifa ya Tanzania au tayari ana Hati
ya kusafiria ya Uingereza
SIKIZA HAPA :
No comments:
Post a Comment